facebook

Sunday, March 31, 2013

Obama plays golf, attends college basketball playoff game

Reuters/Reuters - U.S. President Barack Obama (R) watches an NCAA basketball game between Syracuse Orange and Marquette Golden Eagles in Washington March 30, 2013. REUTERS/Yuri Gripas


WASHINGTON (Reuters) - President Barack Obama had the kind of Saturday that many men dream of having, playing golf and attending a college basketball playoff game.
Midday found him at Joint Base Andrews, the Air Force base on the outskirts of Washington where Air Force One is kept. He teed off at one of the base courses with friends Marty NesbittMarvin Nicholson and Michael Brush.
After a couple of hours, enough to probably play nine holes, Obamahad his motorcade whisk him to the Verizon Center sports arena, where Syracuse defeated Marquette to advance to the semifinals of the National Collegiate Athletic Association men's basketball tournament.
Inside the Verizon Center, Obama ran into Washington Redskinsstar quarterback Robert Griffin III, who is recovering from knee surgery. A tweeted photo showed them chatting.
Obama, a big basketball fan, admitted to reporters earlier in the week that his predictions of the winners and losers in the NCAA tournament had been "busted."

Jeshi lauwa wapiganaji 14 Kano


Wanajeshi wa Nigeria wanasema kuwa wamewauwa watu 14 wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wa kundi la Boko Haram katika shambulio dhidi ya jengo moja mjini Kano, kaskazini mwa nchi.

Msemaji wa jeshi alieleza kuwa mwanajeshi mmoja alikufa katika shambulio hilo, na mshukiwa mmoja alikamatwa kwenye gari lilojaa mabomu.
Ulinzi umezidishwa kukiwa na wasi-wasi kuhusu usalama wa Wakristo wakati wa Pasaka.
Jeshi la Nigeria linasema wanajeshi walishambulia nyumba iliyoaminiwa kuficha wapiganaji wa Kiislamu, baada ya gari kuvuka kizuizi cha jeshi.
Limesema kuwa wanajeshi walikuta silaha na gari lilosheheni mabomu ndani ya uwa wa nyumba hiyo, ambayo iliangamizwa.
Inasemekana shahidi mmoja alimuona mwanamke na mtoto kati ya waliokufa.
Jeshi mara nyingi linapunguza hasara inayopata na linawajumuisha wote waliouwawa kuwa wapiganaji.
Makundi ya kutetea haki za kibinaadamu yanasema wanajeshi mara nyingi wanauwa raia katika operesheni zake dhidi ya wapiganaji.

Cheki video mpya ya Shaa hapa



Mandela aombewa afya njema

Makanisa ya Afrika Kusini yamemuombea rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anatibiwa homa ya mapafu, pneumonia.

Jumamosi msemaji wa rais, Mac Maharaj, alieleza kuwa Bwana Mandela aliweza kuvuta pumzi bila ya shida na amepata nafuu, lakini bado wasi-wasi ungaliko kuhusu kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 94.
Bwana Mandela aliishi mtaa wa Soweto, Johanneburg, kwa miaka mingi.
Mkaazi mmoja wa Soweto, Eddie Vilakazi, aliyemuombea Bwana Mandela katika ibada ya Pasaka Jumapili, anasema anatumai mzee huyo ataishi muda mrefu:
"Mandela ni kiongozi wetu.
Tunamuona kuwa mkombozi wetu.
Ni kila kitu kwetu.
Tunamtakia afya njema haraka.
Mungu amuangalie, ambariki kwa sababu tayari ameshabarikiwa.
Lakini tunamtakia maisha marefu zaidi, awe nasi."

AZMA FT KITA KIPIMO CHA PENZI VIDEO


MY GIRLFRIEND IS MY BEST FRIEND ARTIST:AZMA FEAT KITA

MY GIRLFRIEND IS MY BEST FRIEND
ARTIST:AZMA FEAT KITA

MITINDO HURU TOKA M LAB !


PAKUA VIDEO YA NASH MC - VVU


Hit song kutoka kwa nash mc

WAPOTEEN CLICK

Wapoteen click KIbabu wapoteen/ Keny wapoteen/ Robart wapoteen/G.Rambo Wapoteen.

Kenya shuwari kidogo

Kumetokea ghasia mjini Kisumu, Kenya, baada ya uamuzi wa mahakama makuu ya Kenya kuthibitisha kuwa Uhuru Kenyatta ndiye aliyeshinda uchaguzi wa rais wa Kenya.
Watu wawili walipigwa risasi na kuuwawa katika mapambano baina ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.

Piya kulikuwa na mvutano katika mitaa ya Nairobi inayomuunga mkono Raila Odinga.

Mwandishi wa BBC anasema wakati Kenya inasherehekea Pasaka, piya inaonesha kuwa iko tayari kumaliza kipindi hiki cha wasi-wasi.

Waliotabiri ghasia kama za miaka mitano iliyopita, hadi sasa hazikutokea.

Maswala yoyote yaliyokuwako kuhusu namna uchaguzi ulivyoendeshwa yanagubikwa na hamu ya watu kutaka amani.

Uhuru Kenyatta ameahidi kuongoza nchi kwa niaba ya Wakenya wote.

Itabidi achanganye jukumu hilo pamoja na kesi yake katika Mahakama Makuu ya Kimataifa, ICC.

Atavyoshughulikia kesi hiyo, ndiyo itaamua uongozi wake utavyokuwa siku za usoni

Saturday, March 30, 2013

I Have A Dream: Martin Luther King Jr Day na Harakati Tanzania ya Sasa Kil

             


Kilichonisukuma kuandika post hii ni habari niliyoiona kwenye runinga katika kipindi cha Anderson Cooper 360 (katika kituo cha CNN) kwamba mwanabodi wa taasisi moja ya elimu huko Marekani amekuwa akimshambulia mwanaharakati Dkt Martin Luther Jr,ambaye jana ilikuwa siku ya kumbukumbu yake (Martin Luther King Jr Day). Mashambulizi hayo dhidi ya Dkt King yalijumuisha madai kama "mwanaharakati huyo hakuwa Dokta"-ikimaanisha si sahihi kuweka kitangulizi hicho kabla ya jina lake,na "alikuwa mkomunisti"- na kwa wahafidhina nchini Marekani,ukomunisti
unachukuliwa kama Unazi. Tukio hilo ni mwendelezo tu wa mashambulizi dhidi ya Dkt King hususan kutoka kwa wanaokumbatia hisia za ubaguzi wa rangi.Lakini kama kuna mtu aliyekuwa "obsessed" zaidi na jitihada za kumuumbua Dkt King basi si mwingine bali Mkrugunzi wa zamani wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) J.Edgar Hoover.Inaelezwa kuwa shushushu huyo alijitahidi kadri alivyoweza kufanikisha azma yake hiyo muflis,ikiwa ni pamoja na kurekodi (bugging) maongezi
ya Dk King anayetambulika kama chachu ya mapambano (ya amani) na mafanikio ya Wamarekani Weusi kukubalika katika nchi hiyo (kwa kiasi kikubwa).Hata mafanikio ya Barack Obama,Mweusi wa kwanza kushika nafasi ya urais wa Marekani yanahusishwa kwa kiasi kikubwa na harakati na changamoto zilizoanzishwa na Dkt King. Tanzania yetu ya leo inaweza kabisa kulinganishwa na hali ilivyokuwa katika Marekani ya enzi za akina Dkt King ambapo ubaguzi wa rangi ulikuwa umeshamiri vilivyo.Huko nyumbani,na hasa baada ya kifo cha Baba wa Taifa-aliyekuwa muumini mkubwa wa usawa wa binadamu-wengi wa wanasiasa wetu wamekuwa bize kutengeneza mgawanyiko katika jamii kati ya wenye nacho na wasio nacho,vigogo na walalahoi,na katika zama hizi za Kikwete,tumeshuhudia
mgawanyiko mkubwa zaidi katika jamii; mafisadi dhidi ya wananchi wa kawaida,na hivi karibuni CCM,Serikali yake na vyombo vyake vya dola dhidi ya wananchi na wapinzani (hususan Chadema) na haki zao. Lakini pengine la kutisha zaidi ni vuguvugu linalochochewa na CCM ya Kikwete na mafisadi anaowalea la kuwagawanya Watanzania kwa misingi ya imani zao za kidini.Kila mwenye macho na masikio ameona na kusikia kauli mbalimbali za msigishano kati ya viongozi wa CCM na baadhi ya viongozi wa Kanisa kwa upande mmoja,na kwa upande mwingine ni msuguano (unaoelekea kukua) wa kimtizamo kati ya baadhi ya viongozi wa Kanisa na baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislam. Kama ambavyo nimerejea kwenye posts na makala zangu kadhaa huko nyuma,suala hili tofauti za kidini kutumika kwa maslahi ya kisiasa linanigusa sana,kitaaluma kama mwanafunzi wa utafiti katika mahusiano ya siasa na dini,na kama raia wa Tanzania-nchi ambayo licha ya kuwa na viungo (recipes) vinavyoweza kupelekea mgogoro wa kijami kwa misingi ya kidini,angalau hali kwa ujumla imekuwa salama (kwa maana ya kutokuwepo vurugu za aina hiyo). Inapofikia mahala vyombo vya habari vya umma,kama TBC1,Habari Leo na Daily News,vinatumika kusambaza ujumbe wa kuchochea mvurugano katika jamii badala ya kuhamasisha maelewano,ni dhahiri kuwa tunakoelekea si kwema.Vyombo hivi vya habari vinavyoendeshwa kwa fedha za walipakodi pasipo kujali itikadi zao za kisiasa vinaanza kuchukua mwelekeo wa gazeti la Kangura na vituo vya radio vya Radio Rwanda na Radio Télévision Libre des Mille Collines (RTLM) ambavyo vilichangia sana kuhamaisha propaganda za chuki dhidi ya Watutsi zilizopelekea mauaji ya kimari nchini Rwanda kati ya mwaka 1994-95. Hivi kama blogu binafsi ya Ze Utamu ilipigwa kufuli kwa vile tu ilionyesha picha isiyofaa ya Rais Kikwete,kwanini basi vyombo hivyo vya habari vya umma vinaruhusiwa kuchochea chuki miongoni mwa Watanzania ambapo madhara yake ni makubwa zaidi ya namna picha za Ze Utamu zingeweza kumdhalilisha Kikwete?Hapa sio kama naitetea blogu hiyo bali ninachojaribu kupigia mstari ni ukweli kuwa amani ya Watanzania inayowekwa rehani na TBC1,Habari Leo na Daily News
ina umuhimu na thamani kubwa pengine zaidi hadhi ya Kikwete pekee.Ikumbukwe kuwa wakati jitihada za Serikali kuitia kufuli Ze Utamu zilipelekea picha hizo kutoonekana tena,sumu inayomwagwa na vyombo hivyo vya habari vya umma ikishasambaa hakutakuwa na namna ya kuizuwia. Nirejee kwa Dkt King na funzo linaloweza kusaidia katika harakati za mapambano dhidi ya udhalimu wa Kikwete na CCM yake inayoendeshwa kishkaji.Pamoja na jitihada na nguvu kubwa iliyotumika kumdhibiti,na hatimaye kuuawa,mbegu alizopanda mwanaharakati huyo zimefanikiwa kuzalisha watu kama Obama,Oprah,Condoleeza Rice,Collin Powell,nk ambao kwa hakika wasingeweza kujichomoza katika mfumo wa kibaguzi uliowabagua Weusi katika kila nyanja ya maisha nchini Marekani. Kama ambavyo Dk King aliandamwa na FBI na J.Edgar Hoover ndivyo wazalendo kama Dkt Wilbroad Slaa walivyojikuta wakiandamwa na taasisi za serikali katika kila wanalofanya,huku baadhi ya waendaji wa taasisi hizo wakidiriki hata kuvunja "miiko" waliyojiwekea ili waweze kumshamshambulia Dkt Slaa (rejea kauli ya Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jack Zoka).Na kama ambavyo wabaguzi wa rangi wanavyoendelea kubomoa misingi iliyowekwa na Dkt King,ndivyo Kikwete akisaidiwa na mafisadi anaowalea-plus vyombo vyao vya habari- wanavyofanya kila wawezalo kudhoofisha harakati za kuwakomboa Watanzania kutoka katika himaya ya ufisadi,ukiukwaji haki za binadamu na umasikini wa kupindukia. Usihadaike na kauli za watu kama Lowassa wanajifanya kutahadharisha kuwa mjadala wa Katiba mpya usiwe chanzo cha kuhaarisha amani kwani yayumkinika kuamini kuwa wale wote wanaohusishwa na ufisadi wasingependelea kuona tunakuwa na Katiba mpya inayompa mamlaka mwananchi wa kawaida kuwa mwenye nchi halisi badala ya hali ilivyo sasa ambapo nchi yetu imekuwa kama kampuni binafsi ya mafisadi,wakiipelekesha
watakavyo na sheria zikibaki sheria tu isipokuwa katika kukandamiza maandamano ya amani na kuminya haki za binadamu. Licha ya kuuawa kwake,wengi wa Wamarekani Weusi sasa wanafaidi matunda ya harakati za Dkt Martin Luther King Jr.Vikwazo na upinzani wa kila hali dhidi ya harakati hizo hakukumvunja moyo Dkt King,na hata kifo chake hakiwazuia washirika na watangulizi wake kuendeleza harakati hizo za kudai usawa wa binadamu.Damu ya mashujaa iliyomwagika huko Arusha kutokana na unyama waliofanyiwa na polisi wa Kikwete na IGP Mwema isipotee bure bali iwe chemuchemu ya kudumu kuhakikisha kuwa hatimaye udhalimu na ufisadi wa CCM na serikali yake unakomeshwa completely. Kama Dkt Martin Luther King Jr aliweza,na Nelson Mandela akaweza pia-bila kusahau kuwa nasi pia tuliweza kumwondoa mkoloni na kumfurumisha nduli Idi Amin-basi kwa hakika harakati hizi za sasa zinaweza pia kufanikisha ndoto na malengo yetu ya kuwa na Tanzania tunayostahili kuwa nayo,na sio hii ya sasa inayoendeshwa kwa remote control na mafisadi huku wakiwatuza majambazi wa Dowans kwa mabilioni na "kuwazawadia" waandamaji wa amani risasi za kuwaua na kuwajeruhi.

                   

Balaa tena! Watu 40 wahofiwa kufukiwa baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Dar


Dar es Salaam. Watu zaidi ya 40 wanahofiwa kufukiwa na kifusi baada ya jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa kuporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana asubuhi.

Kuporomoka kwa ghorofa hilo lililokuwa katika Mtaa wa Indira Gandhi, kulizua huzuni, taharuki na simanzi kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye eneo la tukio kutaka kufahamu nini kimetokea.

Shughuli mbalimbali katikati ya jiji hilo zilisimama kwa siku nzima baada ya jengo hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu watano, 13 kuokolewa huku zaidi ya watu 40 wakisadikiwa kufukiwa na kifusi cha udongo wa jengo hilo.



Jengo lililoporomoka

Jengo hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya ‘Lucky Construction Limited’ lilianguka majira ya saa 2.30 asubuhi wakati ujenzi ukiendelea juu huku chini watoto wakicheza mpira na mama lishe wakiendelea na biashara zao kama kawaida.

Pamoja na vifo na wengine kujeruhiwa, magari takribani manne yalifunikwa na kifusi cha jengo hilo na kupondwa pondwa na kuwa kama chapati.

Katibu wa Msikiti wa huo wa Shia Ithnasheri, Mushtaq Damji alisema: “Leo tulikuwa na kitu kama jumuiya kwa jamii ya wahindu, tulipanga kusherehekea lakini yote yakafutika.

“Baada ya swala ya alfajiri, watu walikuwa wanazungumza hapa na pale na baada ya kupambazuka, watoto walikuwa wanacheza mpira, walikuwa 9. Sasa, bahati nzuri watoto saba wakakimbia na watoto wawili wakawa wamekwama,” alisema Damji.

Naye Mlinzi wa Msikiti huo, Athuman Nassor alisema: “Mimi nafanya kazi ya ulinzi hapa msikitini, lakini nilikuwa ninashangaa kiasi cha saruji kilichokuwa kikitumika kukorogea zege, kweli walikuwa wanazidisha mchanga.

“Niliwahi kuwaambia hata hawa vibarua, kuwa hii inayofanyika mbona siyo…,” alisema mlinzi huyo. Alisema; jana ilikuwa siku ya kumwaga zege ghorofa ya 16 na kulikuwa na vibarua wapatao 50 ambao kila mmoja alikuwa na ndoo yake tayari kuanza kazi kabla ya ghorofa hilo kuporomoka.

Mlinzi huyo alisema kuwa wakati tukio hilo linatokea alikuwa mbali kidogo na eneo la tukio na kusema kuwa bila shaka baadhi ya kinamama lishe ni miongoni mwa waliofukiwa.

DARASA kutoka na MILELE ndani ya SIKATI TAMAA ALBUM and (Audio) Shetta ft Rich Mavoko - Sina Imani

NEW SONG FROM SHETTA

Cameron ampongeza Kenyatta





Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron imetoa taarifa iliyosomwa na msemaji baada ya hukumu ya mahakama makuu ya Kenya kuamua kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda kihalali uchaguzi uliofanywa awali mwezi March.

Taarifa zinazohusiana
Kenya, Uingereza, Siasa

Msemaji alieleza kuwa waziri mkuu amemuandikia rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Jumamosi.

Alimpa hongera yeye pamoja na wengine waliochaguliwa ambao ushindi wao ulikubaliwa na mahakama makuu Jumamosi.

Alisistiza kuwa hii inamaanisha mwisho wa mchakato uliokuwa muhimu, ambapo wananchi wengi kabisa walijitokeza kupiga kura kushinda wakati wowote ule.

Waziri Mkuu aliwasihi Wakenya wajivunie ishara waliyopeleka kwa ulimwengu kuonesha azma yao ya kutumia fursa yao katika demokrasi.

Alisema watu wa Kenya wameamua kuonesha uhuru wao na kutatua mizozo kisheria na kwenye taasisi imara ya mahakama makuu, na katiba.

Waziri Mkuu Cameron piya alisistiza kuwa Uingereza imeazimia kuendeleza ushirikiano baina yake na Kenya.

Ameelezea uhusiano baina ya Uingereza na Kenya ni wa kihistoria na wa kina, na anatazamia kufanya kazi


Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki


Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.

Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.
Taarifa zinazohusiana
Kenya

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.

Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao

Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.

Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.

Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.

Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.

Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.

Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.

Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.

Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.

Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.

Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.

Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.

Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo

Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.