facebook

Wednesday, October 9, 2013

Historia ya DUKE TACHEZ: katika safari yake ya u-producer!

DUKE
 Anajulikana zaidi kwa jina la DUKE TACHEZ lakini jina lake halisi ni Duke Gervalius Duke. Alianza kufanya kazi ya kutengeneza Music mwaka 1998 akiwa mtaani tu. Kwa sababu kipindi iko ilikua ni vigumu kuingia kwenye studio kubwa kama Bongo Records.
Duke Tachez alipendelea sana kutengeneza midundo aina ya Hip Hop, na Mwaka 2002 alifanikiwa kuingia kwenye studio Dynamic grooves ambayo alikuwa akishare na rafiki. Ambayo haikujulikana sana kwa sababu ya kufanya kazi nyingi za Undergrounds.

Mwaka 2004 baada ya studio kuanzishwa ambayo ilikua ikiitwa Pinnacle Production wakiwa na producer kutoka kenya Dunga na wakafanikiwa kufanya kazi kama Usipime ya Black Rinno, Temba Ft Ray C – Nipe Mimi, Profesa ft Bamboo – Karibu, Chegge ft Temba – Hili Dude na nyingine nyingi.
Duke hakuishia hapo tu mwaka 2005-2008 akatoka Pinnacle production na akaamua kuwa Producer wa kujitegemea na alifanikiwa kufanya kazi na Studio mbali mbali kama 41 records, Kama Kawa Records, Pasu kwa Pasu records, Dhahabu Records, Bongo Records & Tongwe Records Ambapo alifanikiwa kufanya nyimbo ni ya Wanaume halisi – tatu bila Remix, I am Proffesinal ya Fid Q, Zero – Witness ft Fid Q, O-ten ft Chidi – Nyandindi, Chiku Ketto ft Lameck Ditto – Muda Umefika, Ripoti za Mtaani Fid Q ft Zahiri Zorro, Traveller ya Solo Thang, Babuu wa kitaa – Wa Kitaa.
Duke pia alifanikiwa kufanya Mixtape KITAANI VOL 1 ambayo ilikua na collection ya baadhi ya nyimbo ambazo aliwahi kufanya akiwa kwenye studio mbali mbali.

DUKE

No comments:

Post a Comment