Baada ya polisi kufanya msako mkubwa mjini Boston, Marekani, wamemkamata mtu wa pili anayeshukiwa kushambulia marathon ya Boston kwa bomu.
Kijana huyo alikutikana amejificha kwenye mashua baada ya mtu mmoja aliyeona mchirizi wa damu kuwazindua polisi.
Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 19, na anayetoka katika eneo karibu na Chechenya, Urusi, Dzhokhar Tsarnaev, alikamatwa baada ya kufyatuliana risasi na polisi.
Amejeruhiwa vibaya na anatibiwa hospitali.
Wakaazi wa mtaa huo walipiga makofi na kushangilia wakati anaondoshwa na polisi kwa gari.
Rais Obama aliwasifu polisi na watu wa Boston kwa uvumilivu wao wakati wote wa shambulio na msako.
Piya alisema ni wazi kuwa washambuliaji wameshindwa.
Alisema watu wanataka kujua kwanini shambulio hilo limetokea:
"Bila ya shaka kuna maswala mengi hayakujibiwa.
Moja ni kwamba kwanini vijana waliokulia na kusoma hapa, wakiwa sehemu ya jamii yetu na nchi yetu, wanafanya kitendo cha maafa kama hiki?
Walipanga vipi na kutekeleza mashambulio hayo?
Na jee walisaidiwa?
Familia za wale waliouliwa kiholela wanastahiki kupata jawabu.
Majeruhi ambao baadhi yao sasa inabidi wajifunze kusimama, kutembea na kuishi tena wanahitaji jawabu.
Kwa hivo nimeliambia shirika la upelelezi la FBI na Idara ya Usalama wa Taifa na maafisa wa ujasusi kuendelea kutumia njia zote
Saturday, April 20, 2013
Monday, April 15, 2013
Milipuko yaitikisa Boston Marathon

Milipuko miwili katika eneo la kukamilisha mbio ndefu za Boston imesababisha majeruhi wasiojulikana idadi yao.
Picha na video kutoka Boston zinaonyesha watu wakiwa wamechanganyikiwa wasijue pa kwenda, huku magari ya huduma za dharura yakielekea katika eneo la tukio na watu waliojeruhiwa vibaya wakipelekwa kwenye hema la matibabu ya haraka.
"Kuna watu wengi wamelala chini," alsiema mwanariadha mmoja akinukuliwa na chombo cha habari cha AP.
Tukio hilo linaripotiwa kutokea saa tatu baada ya washindi kuvuka mstari wa ushincdi.
"Kulikuwa na mlipuko, polsi, moto na EMS kwenye eneo latukio. Hatuna namna ya kutulekeza namna watu walivyojeruhiwa," msemaji wa Polisi Boston alisema.
AP linasema kulikuwa na sauti kubwa ya mlipuko upande wa kaskazini mwa mtaa wa Boylston Street, karibu tu daraja linaashiria mstari wa kumalizia mashindano. Mlipuko mwingine ukasikika dakika chache baadaye.
Mike Mitchell wa Vancouver kutoka Canada, mwanariadha aliyemaliza kukimbia alisema alikuwa akiangalia nyuma ya mstari wa kumalizia mashindano ndipo aliposikia ‘mlipuko mkubwa’
Inataarifiwa kuwa moshi ulipanda juu hewani kiasi cha futi 50 (mita 15),' aliliambia shirika la habari la Reuters , na watu wakaanza kukimbia wakipiga mayowe baada ya kusikia
"Kila mtu alichanganyikiwa,’ alisema.
Waliokuwa wakimalizia mbio hizo waliongozwa kuepuka eneo lenye moshi kwenye mlipuko wakati huo huo eneo hilo likifungwa.
Tawi la Msalaba Mwekundu la Mashariki mwa Massachusetts limetenga kituo cha kusaidia majeruhi.
.
Mahakama yaamuru Mubarak asizuiliwe tena.
Mahakama ya rufaa nchini Mirsi imeamuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak hapaswi kuzuiliwa tena kuhusiana na vifo vya waandamanaji waliofariki wakati wa mapinduzi yake.Lakini Mubaraka atasailia kizuizini huku uchunguzi ukifanywa kuhusiana na kesi ya ulaghai dhidi yake. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali Misri
Taarifa zinazohusiana
Siasa
Mahakama ya rufaa mjini Cairo iliamuru hilo ikisema kuwa Mubaraka amezuiliwa kwa miaka miwili kipindi kinachoruhusiwa cha mshukiwa yeyote kuzuiliwa kabla ya kesi kusikilizwa na kuamuliwa.
Kesi dhidi ya Mubarak itasikilizwa tena huku akitaka uamuzi wa kufungwa maisha jela kubatilishwa.
Aidha Mubarak,aliyetawala Misri kwa miongo mitatu aling'olewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mwaka 2011.
Amekuwa akizuiliwa tangu Aprili mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na vifo vya mamia ya waandamanaji waliofanya maandamano ya amani wakimtaka aondoke mamlakani Januari kati ya tarehe 25-31.
Pia anakabiliwa na kesi ya ufisadi.
Mawakili wake walitaka mahakama kumwachilia Mubaraka kwani amezuiliwa kwa miaka miwili sasa na kulingana na sheria anapaswa kuachiliwa ikiwa kesi yake haijaamuliwa.
Wednesday, April 10, 2013
Watoto, ''wadhulumiwa sehemu za vita''
Shirika la kuwahudumia watoto la Save the Children, linasema kuwa watoto ndio waathiriwa wakubwa wa
ubakaji na dhulma zengeine za kingono katika maeneo ya vita duniani.
Ripoti ya shirika hilo inazingatia data waliokusanya pamoja na ushahidi kutoka katika nchi nyingi ikiwemo Colombia, Liberia na Jamuhuri ya kidemorasia ya Congo.
Taarifa zinazohusiana
afya
Save the Children linasema kuwa mipango mingi au miradi ya kusitisha dhulma hizo na kusaidia watoto huwa hazipati ufadhili wa kutosha
Swala hilo litajadiliwa na mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la G8 au la nchi zilizostawi kiviwanda.
Uingereza ilisema kuwa itatoa kipaombele kwa swala la dhulma za kingono katika maeneo ya vita wakati wa uongozi wake wa G8 mwaka huu.
Ripoti hiyo ya Save the Children, yenye kauli mbiu, Dhulma za kinyama dhidi ya watoto, inasema kuwa takwimu kutoka katika nchi kadhaa, zilizoathirika kutokana na vita katika miaka kumi iliyopita, zinaonyesha kuwa watoto ndio hudhulumiwa zaidi kingono katika maeneo ya vita na hata baadaye.
Makovu ya kudumu
Utafiti uliofanywa nchini Liberia, ulionyesha kuwa asilimia 83 ya waathiriwa wa dhulma hizo, kati ya mwaka
2011-12 walikuwa chini ya umri wa miaka 17 na takriban wote walibakwa.
Nchini Sierra Leone, baada ya vita, zaidi ya asilimia 70 ya unyanyasaji wa kingono ulifanyiwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 18, na zaidi ya nusu yao walikuwa chini ya umri wa miaka 11.
Katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, takriban thuluthi mbili ya visa vya ubakaji vilivyorekodiwa na UN mwaka
2008, vilihusisha watoto na wengi wao wakiwa wale waliovunja ungo.
Wasichana na wavulana wanatekwa nyara na kudhulumiwa na wanajeshi pamoja na makundi ya wapiganaji , kwa mujibu wa shirika hilo.
ubakaji na dhulma zengeine za kingono katika maeneo ya vita duniani.
![]() |
WA TOTO |

Miili ya polisi waliouawa Nigeria yapatikana
Maafisa wa usalama nchini Nigeria wamepata miili 11 ya wanajeshi 12 waliouawa katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta siku ya Ijumaa.
Polisi wanasema kuwa baadhi ya miili hiyo ilikuwa imekatwakatwa na kuchomwa kiasi cha kutotambulika.
Taarifa zinazohusiana
Siasa
Wiki jana kundi moja la wapiganaji, lilisema kuwa litaanza mashambulizi mapya baada ya kiongozi wake Henry Okah, kufungwa jela kwa kufanya shambulizi la bomu mwaka 2010.
Eneo hilo lenye utajiri wa mafuta, ni muhimu sana kwa uchumi wa Nigeria.
Hata hivyo, watu wengi ni maskini na hivyo huchukizwa na serikali pamoja na makampuni ya mafuta kwa kutowafaidisha na rasilimali hiyo.
Mwishoni mwa wiki, kundi la wapiganaji wa MEND, walisema kuwa walivamia mashua iliyokuwa imewabeba polisi katika jimbo la Bayelsa na kuwaua polisi.
Msemaji wa polisi, Alex Akhigbe alisema kuwa miili 11 zilipatikana wakati polisi mmoja hajulikani aliko.
Miili hiyo ilisafirishwa kwa boti hadi katika eneo la Yenagoa ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo kuchukuliwa na familia zao.
Aidha mwishoni mwa wiki polisi walikana kuwa mauaji hayo yanaweza kuhusishwa na kufungwa kwa Henry Okah.
Badala yake walisema kuwa yalihusu mgogoro wa malipo ya mishahara ya wapiganji hao waliokuwa wanalipwa baada ya kukomesha harakati zao za mapigano dhidi ya serikali.
Mashua za polisi waliokuwa wanamsindikiza mwenzao kwa mazishi, zilikumbwa na hitilafu na hivyo kulengwa na wapiganaji hao kwa mashambulizi.
Kundi la Mend lilikuwa linafanya vurugu kutaka kupewa sehemu ya rasilimali za mafuta Kusini mwa Nigeria lakini likasitisha harakati zao mwaka 2009, wakati waliposalimisha silaha na kusamehewa.

Tuesday, April 2, 2013
Coming Soon: ‘Kwanza FM’ kituo cha radio mali ya Lady Jaydee.
Hatimaye tumepata jibu la kwanini Judith Mbibo aka Lady Jaydee amekuwa akitweet vitu vizito weekend iliyopita. Kama hukufaniwa kuziona tweets hizo ni kwamba mwanadada huyo alishusha mfululizo wa mabomu kuelekea kwa kituo kimoja cha radio na kujikuta akiongeza aka mpya, Anaconda.
Na sasa imebainika kuwa mwanamuziki huyo mkongwe na mjasiriamali anakuja na kituo chake cha radio kiitwacho Kwanza FM. Habari hiyo aliibreak mwenyewe jana na bila shaka haihusiani na April’s Fools Day.

Kwanza FM coming soon. Yangu mwenyewee
— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013
Inaonesha kuwa mchakato wa kuanzisha radio hiyo unaenda vizuri kiasi cha kuweka wazi na kuwa hiyo ndio sababu alichukua uamuzi huo wa kuandika mambo ambayo yangeweza kuiharibu career yake ya muziki.
Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea— Lady JayDee (@JideJaydee) April 1, 2013
Kila lakheri Lady Jaydee. Kwa usimamizi wa mumewe Gadner G Habash ambaye ana uzoefu mkubwa kwenye masuala ya radio, kituo hicho huenda kikafanya vizuri.
Monday, April 1, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)