facebook

Saturday, June 29, 2013

NEW T-SHIRT MGOLOKO ZIKO MTAANI SASA!








Wapoteen click watoa T-shirt za Mgoloko na ziko mtaani sasa kama unahitaji wasiliana na G.Rambo Wapoteen 0717652551/Kibega Wapoteen 0717774040/Kibabu Wapoteen 0716440140!

Thursday, June 27, 2013

Hali ya Mzee Mandela inaendelea kuzorota!



Ujumbe kwa Nelson Mandela
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac Maharaj amesema kuwa hali yake imedorora zaidi katika saa 48 zilizopita.
Mandela ambaye, ni rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8 mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu hali ya Mandela.
"tutasikitika sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijana John Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua kuakhirisha safari yake.
Taarifa kutoka kwa ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika Kusini wanaoendelea kuiombea familia ya Madiba.
Uamuzi wa Rais Zuma kufutilia mbali ziara yake ambako alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa kikanda kuhusu uekezaji anaonyesha wazi kuwa hali ya Mandela inaendelea kuzorota zaidi kulingana na mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Mike Wooldridge.

Rais Obama atua Senegal kwa ziara Afrika!



Hi ni ziara ya pili ya Rais Obama Afrika
Rais Barack Obama amewasili Senegal katika ziara yake ya wiki moja barani Afrika na anatarajia kuzuru Afrika Kusini na Tanzania akilenga kustawisha demokrasia na masuala ya uchumi.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hata hivyo ziara yake inatarajiwa kufifishwa na hali mbaya ya afya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela. Ikulu ya white house imesema kuwa itategemea uamuzi wa familia ya Bwana Mandela iwapo Rais Obama anaweza kumtembelea hospitalini.
Katika mkutano wake wa leo na rais wa nchi hiyo, Mackey Sall, Rais Obama anatajiriwa kuipa heko Senegal kwa rekodi yake nzuri ya uthabiti ikizingatiwa iko kwenya kanda yenya misukosuko ya kisiasa.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa muhimu katika ziara ya Obama ni kustawisha demokarsia na nchi zote tatu anazotembelea ziko na demokasria thabiti.
Ni ziara ya pili ya Obama katika bara la Afrika tangu kuwa rais wa Marekani mwaka 2008.

Monday, June 24, 2013

Walimu watangaza mgomo rasmi Kenya!


Walimu wanataka serikali kuwalipa marupurupu waliyokubaliana tangu mwaka 1997
Chama cha kitaifa cha walimu nchini Kenya, kimetangaza mgomo wa kitaifa kuanzia leo baada ya serikali kukosa kuwalipa marupurupu yao.
Huu ni mgomo wa saba wa walimu tangu mwaka 2007.
Mwnyekiti wa kitaifa wa chama hicho,Wilson Sossion alituhumu serikali kwa kucheza siasa na maswala yanayowahusu walimu kwani wanafahamau masaibu ya walimu na mkataba wa mwaka 1997 uliotoa ahadi ya marupurupu hayo kwa walimu.
Kulingana na makubaliano hayo, serikali inapaswa kuwalipa walimu marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu , kuwlaipia nyumba , matibabu na pesa za usafiri.
"tumedurusu mienendo ya serikali na kugundua kuwa wantumia mtindo wa kugawanya watu. Hilo halitafanya halitafaulu,'' alisema bwana Sossion
"tumetangza kuwa mgomo wa waalimu unaanza rasmi leo, '' aliongeza bwana Sossion
Sossion pia alisema kuwa tume ya kushughulikia maswala ya walimu, haina mamlaka ya kuwaamuru walimu kutogoma au vinginevyo kwani hilo ni jukumu la Knut.
Katibu mkuu Knut, bwana Nyamu aliseama kuwa chama cha walimu kimeweka bayana matakwa yao waliyokubana na serikali mwaka 1997.
"marupurupu haya yote sharti yalipwe.Tumekwenda kwa wizara ya limu ya kuelezea malalmiko yetu,'' alisema bwana Nyamu.
"tunawaambia walimu kuwa katibu mkuu atawapa maagizo kuhusu watakachofanya wakati wa mgomo huu. Walimu waanze kwa kukabidhi majukumu yao katika shule zao leo.
Nyamu pia aliwataka walimu kuwaondoa watoto wao shuleni kwani walimu hawatakuwepo kuwafundisha.
''Kwa sasa tunaiacha serikali ifanye uamuzi , tutaketi chini na kusubiri,'' alisema Nyamu
''Wanachokitaka walimu ni pesa, na wale wanaomshauri rais wamwambie kuwa lazima walimi wapewe pesa kwani hawatazungumzia kingine ila marupurupu yao,'' alisema Sossion

Sunday, June 23, 2013

IFAHAMU HISTORIA YA MUZIKI WA HIP HOP ILIPOANZIA HUKO MAREKANI!

MAKALA IMEANDIKWA KWA KINGEREZA ILA NIRAHISI KUITAFSIRI KAMA UTAPENDA KUTAFSIRI.........songa nayo,....
The hip hop period is divided into two eras-the old school hip hop (1970-1985) and the golden age hip hop (1985-1993). The hip-hop style is actually very famous and popular in the USA. Hip hop involves rapping, break dancing and is also very popular because of the style of dressing. It is believed that hip hop originated in the Bronx by Kool Herc who was a Jamaican DJ. He was amongst the earliest to gain fame. In hip hop music, the singers individually vocalize over the beats. The old school hip hop artists always focused on introducing themselves and even the guests over the music. Later, this presentation got more varied and the approach was more rhythmic with rhyming lyrics from the African American culture.
Hip hop music has originated from the African American and the West African music. There was a lot of funk and soul music being played during the old school hip-hop era. The golden age hip hop era saw rappers such as Big Daddy Kane and Kool G Rap. The new school of hip hop culture also saw the duo Jazzy Jeff and the Fresh Prince bag the first rap Grammy Award. This was the period that saw the emergence of new hip hop styles. For the first time in the history of hip hop, it was combined with rock, reggae and even techno music. Rap formed a major part of hip hop and also the dance and the clothing styles achieved prominence. The all female group, Salt ‘N’ Pepa tasted stupendous success with singles such as the ‘The Show Stoppa’. The interests in the rap music saw a steady rise and there were various messages that were incorporated in the hip hop music such as stories on crime, drugs and violence. The street language was passed on to the hip hop culture through rap music..         
The hip hop dance gained popularity as it offered a platform to express one’s creativity. Hip hop gave one a chance to dance freely without adhering to the rules that is required in ballroom and ja
style of dancing. Breakdance formed the base for hip hop dance. This appeared in the early 1960s in the New York City. The different styles of hip hop dance includes the harlem shake, snap dance, grinding, gangsta walking, soulja boy, krumping etc. Along with the dance, the hip hop style of dressing also gained popularity along the way. The hip hop look was never complete without baggy jeans, loose Tees, chunky jewelry and loads of bling. This is because, hip hop is not just about dance and music but is a culture in itself. The hip hop dance can never be complete without the right style of hip-hop clothing. Hip hop fashion has cut across all boundaries since the olden days. Today, apart from the loose attire, the women are known to sport fitting skirts with legging and layered tops with gold lockets to make a style statement
Gangsta rap saw success in the year 1986. This was mainly because of the very popular "6n’ Da Mornin'" by Ice T. This gangsta rap trend influenced more groups along the way such as Puff Daddy, Snoop Doggy Dogg, Dr. Dre and The Notorious B.I.G. etc.
Hip hop therefore has generations of fan following. We can see how hip hop music and the hip hop culture has evolved since the olden days. Many argue that the present style of hip hop may not always reflect the pure form. But despite all the disagreements, one cannot argue with the fact that the hip hop is immensely popular even till date... say steven m....
get rich of selfness....

Saturday, June 22, 2013

MANDHARI YA VINA MPAKA UCHINA!


Najaribu kutoroka nibatue haya makufuli, na kukata minyororo yenye kutu za muda ili nifunguke na shairi la ‘Vina Mpaka Uchina’. Laiti ningekuwa na fursa ya kupata wasaa toka kwenye kurasa hizi adhimu, ningeweza huandika hata kurasa mia mbili; kuzungumzia wimbo huu tu, ama mashairi ya hawa jamaa wa Miraba Minne.
Hili shairi lina aina ya mirindimo, sauti na fikra zinazonifanya niwaze. Kipindi kama hiki niwe na jamaa zangu wote, tumekaa pamoja maeneo fulani hususan Temeke, tunasikiliza huu wimbo kwa mshindo, sauti kubwa sana, labda kwa Juma Chaki (TMK Vetinari) pale au kona ya kwa Gogi.
Tunasikiliza tu, hatuongei wala nini, tunacheka tu na kugongeana, sababu maneno yanaingia moja kwa moja moyoni. Tunanesa na ute mzito wa besi, najifuta jasho la msimu wa kiangazi, tukibugia vumbi la mkito wa huu mdundo. Tunanesa na masingi ya snea za kutu, huku vibarua wa Kioo Limited wakigeuka mdogo mdogo kurejea makwao. Sahani (hi hat) zikitatarika sawia na milio ya ndala za wapitao.
Mirindimo
Ushuhuda wa mirindimo ya besi unanisafirisha hadi utotoni nilivyotoroka kwenda kwenye ngoma ya Tokomile pale kwa Mama Zakia, Kigamboni Raha Leo. Kabla miembe iliyotukuka haijakumbwa na maangamizi ya njozi za maendeleo.
Tokomile ni ngoma ya wakubwa; huyu Teknohama aliyenyonga huu mdundo, ameamsha hizo hisia. Yaani besi inashabihiana na ngoma kuu inayoitwa Mlungula, unaopigwa na pandikizi la jitu (jitu la miraba minne). Hapo wababe wako na bakora zao na kila mtu ana puchali (jisu kubwa) kubwa kiunoni. Kwenye wimbo huu kimekosekana zumari tu, vinginevyo ingeleta madhari fulani matata sana. Unafahamu zumari ina mazingara mengi sana…
Nyanda za Ulimwengu
Maneno yanayosemwa kwenye ‘Vina Mpaka Uchina’ yananifanya nipate hisia ya kwamba, waliopo ulimwengu yabisi na wale waliopo ulimwengu ambao sio yabisi sote tujumuike ili tuburudike kwa pamoja. Wale waliopo ulimwengu si yabisi ni rahisi kufika hapa. Tayari tuko nao na hivyo kwao nasema ‘M.A.P. (Mungu Awaweke Pema)’. Ushanifahamu bwana?
Na wale walio katika ulimwengu yabisi, lakini bahati mbaya wako maeneo tofauti tofauti. Unajua upepo wa muda umetuzungusha na dhoruba zake, kila mtu yuko kona nyingine. Kuna walio Uchina, kama vile wimbo unavyoitwa ‘Vina Mpaka Uchina’, walio Bara la Ulaya, walio huko lizamako jua na kuandamia mwezi — sisi zamani tulikuwa tunawaita Wanyamwezi, siku hizi ni taifa jipya la Wajaluo kwa bwana Baraka Hussein wa Obama — wengine wako Australia na maeneo mbali mbali ya dunia. Wote tunajumuika kusikiliza hizi ngano za kitaa.
Vina Mpaka Uchina vinanipa mandhari ambayo ninaiona kabisa; nipo maeneo ya Salamanda (Mtaa Samora/Mkwepu, Dar) kabla jengo lililokuwepo pale halijakumbwa na dhoruba ya fitna za ukuwadi wa soko huria, kuna kijiwe tulikuwa tunakiita Ngazi Tano… Bado tumo kwenye maudhui ya Vina Mpaka Uchina na natumai tunakwenda sambamba.
Dimbwi la Kumbukumbu
Fitna za makuwadi wa soko huria zimesababisha majengo mengi kuvunjwa, hivyo mandhari ya mji mtukufu wa Mzizima (leo hii tunapaita Dar Es Salaam) imeanza kutoweka.
Huu wimbo unanirudisha siku fulani pale maeneo ya Salamanda, ndio kwanza narejea baada ya kusukumwa na upepo wa muda hadi linakozamia jua na kuangaza miali ya ajabu wakati wa kipupwe, huko Kaskazini ya Mwisho, Kanada. Nikagumiana na wana wawili wa kitambo sana, Yusef Wamba na Hashim Dogo. Sasa, katika ujenzi wetu na shauku yangu ya kutaka kujua fani, Dogo akaniambia ‘hatufanyi tena sanaa’.
Mi’ nikahamaki hapo nikasema, ‘n’take radhi bwana, we una mamlaka gani ya kustahafu kabla yangu, hii kweli heshima?’ Huyu bwana anaitwa Hashim Dogo na wakati wa ujenzi Yusef Wamba (wa Raiders Posse) alikuwepo pembeni yake. Hawa jamaa siwataji tu kiwepesi. Hawa ni watu mahiri sana kwenye huu ujenzi, na itasaidia wadau wengine wa fani kuona ninavyohusiana nayo.
Ikabidi niendelee kumuasa ya kwamba ni utovu wa heshima ya kitaa. Na kwa sababu yoyote inayonizuia mimi nisistahafu, basi yeye pia hana mamlaka ya kustahafu kabla ya mimi kufanya hivyo. Nikasisitiza kuwa hilo sio ombi bali ni amri.
Kwa vile heshima ya kitaa bado ipo, basi baada ya kutafakuri tukafikia muafaka. Kwa hiyo, tukatakana radhi na tukakubaliana kuendelea kujenga na kutumia njia mbadala za kuienzi hii fani. Kuwataja hao jamaa ni kuonesha kuwa lile jopo nitakalokuwa nimesimama nalo pale kwenye kona kwa Gogi, au kwa Juma Chaki TMK, au tuseme Salamanda Ngazi Tano (ambapo bahati imelinusuru jengo hilo), pembeni babu Kheri yupo na majarida bwena, m’ziki mnene… Hiyo ndio mandhari ninayopata ninaposikia mirindimo Vina Mpaka Uchina.
Twend’zetu
Sasa nirudi kwenye mada yetu, ngoja nikuongoze kwenye ulimwengu wa ngano za kitaa kupitia shairi la Vina Mpaka Uchina. Kwenye mstari wa kwanza Nash anaanza na kuingia na mantiki kwa mbali inayoshabihiana na athari za Shaaban Bin Robert. Nash amejitwika jukumu la ualimu, ilhali amekimbia darasa lake (la fani), hapa ameonesha anaweza kutengeneza hoja atapokabiliana na malenga.
Hii mantiki ya uandishi itagusa kwenye changamoto na mijadala mingi inayohusu ngano mbalimbali za ushairi. Sitaingia ndani sana kufikia labda mashairi ya Bi. Mwana Kupona (mshairi wa mahiri kale wa Pwani ya Mwambao wa Ukushi ya Mashariki, karne ya 17) au Fumo Liongo (mshairi mahiri wa kale Kanda ya Mwambao Ukushi ya Mashariki, karne ya 12), bali nitadodosa machache niyajuayo kadri ya uwezo wangu.
Kumekuwepo na mvutano baina ya ngano za mapokeo na ngano huria — sasa huu mfumo wa kupitia Hip Hop, mimi nauita ‘ngano za kitaa’. Kwenye miaka ya karibuni, enzi za Mohamed Ali Kibao, Mulokozi na Kezilahabi, kulikuwa na kambi mbili, ile ya mashairi ya mapokeo na mashairi huria. Mimi napenda kuwepo katikati ya hizi mantiki mbili. Navutiwa na mashairi ya mapokeo na bado safari yangu ya kujifunza bado ndefu sana. Wakati huo huo, upande huria naupokea ila kwa hadhari ya kanuni zitumikazo.
Sitokuwa na ule ‘ushabiki wa Kiulaya’ wa kuwa msanii anayechovya brashi kwenye rangi kadhaa na kuikung’utia kwenye ukuta, na baadae kazi kuuzwa kwa gharama za ajabu, la hasha. Hupenda kuwa na uzuri wa mambo ninayopenda, kuutambua kiuyabisi na kinadharia — yaani kifikra. Hivyo nakusihi uje nami msomaji. Hapa nasema twend’zetu, nataka nisikuache; uje usikie ule mpelampela wa mabomu ya Gongo la Mboto, mayowe ya wapiga debe na honi za daladala zinavyoweza kujibainisha kwenye mfinyango wa midundo ya kaka Teknohama, ambaye ni muandaaji wa mdundo wa wimbo huu, na ni mkazi wa Gongo la Mboto.
Kundi Hili
Miraba Minne ambayo ni mjumuiko wa wasanii binafsi wanne: Nash, PMC, Zaiid na Songa. Ni mkusanyiko wa vitongoji kadhaa vya jiji la Dar es Salaam. Nadhani juhudi hii waliyoifanya ni kuwahakikishia vichwa wa Hip Hop kuwa, ule uvumi uliokuwa ukienezwa kwamba Hip Hop ilihama Dar nyakati fulani ni porojo tu. Na ushahidi unajidhihirisha humu kwenye Vina Mpaka Uchina.
Na kwamba, hao washabiki walifunikwa tu na wingu la hadaa na upepo wa vina vya kitaa vilivyosukumwa sitiari za mbinde za msako wa ugali wa kutwa — vina vya mazingira hatarishi vimeweza kusukuma hilo wingu na hata mvua ikashindwa kunyesha. Huu muundo wa uandishi si mpya. Ni athari bayana za kizazi cha awali kwenye fani ya Hip Hop Tanzania, hususan Kwanza Unit. Hawa jamaa wanaandika kama wanachora na taswira inakuja na muundo wa nyanda tatu, ama ‘3D’ kwa lugha ya kigeni.
Nash
Ukavu wa sauti ya Nash nauhusisha moja kwa moja na lile vumbi la mtaa wa Mkamba, jirani na magereji ya Temeke Hospitali na maeneo yote yanayozunguka TMK, vumbi la sumu la viwandani kama Kioo Limited., Mabati na kadhalika. Ingawa Nash si muumini wa kudumu, athari za mila za Kiislamu zinasikika bayana, “Hii kasida si ya kuimba, tunaghani kiama”. Pia jina la wimbo (Vina Mpaka Uchina) yawezekana kuwa ni kumbukumbu za hadithi za masahaba wa Mtume, kama Ibuni Maja aliposema kuwa Mtume aliwataka masahaba zake na waumini wakaifuate elimu hata Uchina.
Nash anadhihirisha umahiri hapa: “Safina linakuacha, Maalim chata, haswa kwa darasa la Hip Hop; na hata madrasa alifu be, aisee shika ujiti nikubariki kinasa”. Hapa namuona kabisa Samia X na KBC wanachekea hadi wanashika mbavu na kusogeza wimbo nyuma. Maana sisi (jamii ya Kwanza) tunaita hii ‘kutoroka’; hapo alipomaliza ‘alifu be’ kawaida wengi wangetarajia amalize na ‘te’, jamaa akahama kabisa, akasema, ‘aisee shika ujiti!’ Ushaona eeh?
Songa
Bado kidogo Songa anichanganye maana kwenye mizunguko yangu ya awali sikumsikiliza kwa makini. Nilikuwa namvuka na kusikiliza majina niliyoyazoea. Sasa nikatega sikio mara moja, mwanzo ule mstari anavyoanza nilidhani anasema, “Vina mti ulio bora…” Akanihamisha, nikaona kama ameanza na kisa cha Adam na Hawa.
Baadae nikahakiki na kuelewa kuwa ni: “Vina, mke uliye bora”. Amegeuza vina kuwa mkewe na anamuusia. Hapo mwenyewe nilizimika. Hizi tafsida si mambo yanayokuja kiwepesi kama watu wanaoandika vimistari uchwara. Jamaa wanachimbuka mno kuweza kutengeza mistari mepesi madhubuti.
Songa ametokea kitongoji cha Tegeta, kwa wafahamu wa mambo, si habari mpya kuona isimu ya ushairi na mwambao wa Bahari. Sitaki kuongelea nadharia ya kuwa bahari yenyewe ndio inayosababaisha kuwepo ushairi mwambao, ila najua fika kuwa mazingira ya ushairi na mwambao ni jambo lenye isimu moja.
Sasa Songa kutoka Tegeta, ukijumlisha kuwa ni mwambao wa bahari, na yale mazingira yaliyopo kule lazima yanatengeza aina fulani ya fikra. Songa kama kabila nampa Uzaramo, maana ndio hugumzwa kuwa wana maneno mengi. Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya ushairi Songa anadiriki kuisemesha taksi bubu: “Huu ni m’da wa kutubu, hadi taksi bubu leo itasema; nahusudu wema wa Mungu, naabudu kwa nguvu njema.” Kuna vile vina vya mumo kwa mumo ambavyo huleta ladha sana kwenye michano.
ZaiiD
Zaiid ni mzawa wa Mwenge, amezaliwa na kukulia Mwenge. Alipokulia ni mwendo wa dakika tatu wa mtu mzima toka ukumbi maarufu sana wa Mpakani Baa. Hapa ndio makao makuu ya ‘Kamanyola Bila Jasho wana wa Makwizi (Marqueez) du Zaire’. Yeye bila kujua huenda amepandikizwa huu uwezo wa michano ya kimirindimo.
Miezi 9 yake yote kabla ya kuzaliwa, miziki ilikuwa ikilia pale kwa sauti ya juu sana. Mitambao yake si namna zilizozoeleka kwenye redio kwa zama hizi za utandawizi, na ndio maana watu hata wasioongea Kiswahili bado huvutiwa na kumtafuta na kufanya naye mahojiano. Fader ni gazeti mashuhuri sana Marekani, hata mimi nilishtuka nilipopigiwa simu na waandishi wa huko baada ya Zaiid mwenyewe kukosekana hewani kwenye namba yake ya Tigo.
Ule utundu wa kujitafsidisha na ngono ni namna ambayo bado itawasumbua sana wabadilishaji CD na watangavyaji (watangazaji wazinguaji) wa zama hizi, maana thamani ya ushairi ni jambo ambalo linatakiwa liwe kwenye damu ili kupata ladha zake kwa ufasaha.
Wengi wanaweza wakanasa kwenye mtego wa kishairi pale Zaiid anaposema, “Chana Kiingereza, mbongo utaishinda London? Nawapa kav’ kav’ ka’ tendo bila kondom.” Zaiid anaweza akakufanya udhani anaongelea ngono tokea alivyoanza, kwa kuwa amekaa kwenye maudhui hayo hayo. Nilichogundua ni kuwa Zaiid anaonesha jinsi alivyopania kujitoa muhanga; ngono bila kinga inasadikiwa ni kama kujiingiza kwenye balaa linaloweza kukufupishia maisha. Wakati huo huo anaasa, upande mmoja ubaya wa tendo hilo, huku akionesha alivyojitosa kuilinda na kuienzi fani ya Hip Hop na ushairi wa Kiswahili.
Namna alivyoshabihisha neno ‘London’ na ‘kondom’, ni somo linaloweza kusaidia wasioelewa vina. Kwenye hali ya kawaida hayo maneno huwezi kuyatumia hivyo, ila kwa mbinu ya matamshi iliyoshamiri, yeye ameifanya imekaa mule mule. Vina ni namna maneno yanavyotamkwa na mshabihiano wa kusikika na sio herufi tu kama wasanii wengi wanavyodhani. Zamani kwenye Hip Hop Marekani kulikuwa na msemo maarufu “You know the flava?”; anayeambiwa ama kuulizwa anaelewa ladha?
P The MC
Ninasikia bayana uimara wa vyuma vya reli aingiapo PMC, ukiona mchanaji anakwambia jambo ujue kuna namna anashabihisha, “Zima taarab weka Hip Hop; emcee mwenye ghadhabu nishafika, mchezo tafu basi chap chap kata nyika; ila ukicheza rafu nakupiga stop kama FIFA.”
PMC anawakilisha Kiwalani, na sistaajabu anapojiita bohari ya vina: “Unapigwa kwa mistari mi’ nd’o bohari ya vina; na nikishakuacha chali mentali habari sina”. Kiwalani imezungukwa na reli ya Tazara upande wote wa kaskazini hadi mashariki, upande wa magharibi ni eneo la uwanja wa ndege. Kiwalani ni moja ya maeneo ya watu waishio maisha ya mchaka mchaka. Maeneo ya namna hii huwa na athari ya moja kwa moja kwa jamii. Mara nyingi haya hujitokeza kwenye sanaa za ubunifu.
PMC toka nilipomsikia na kukutana nae kwenye WAPI hakuwahi kuniangusha, ni moja ya wasanii nilioona wazi kuwa ni hazina ya Hip Hop.
Hatimaye
Kiukweli siwezi kumaliza uchambuzi wa huu wimbo kwa makala moja. Nikipata fursa nitajaribu kuchambua beti hadi beti. Pia, kwa utashi wako msomaji, nia ya makala kama hizi ni kuonesha ama kuibua lulu ya fani iliyopo chini kabisa ya vina virefu. Kwa vile pumzi ninayo na maji nimeshayavulia, acha kwa leo niogelee humu humu tu na nikirejea nitakuwa nimeshaibuka toka mbizi au chomo (neno jipya nimejifunza toka kwa Songa) ya kuibua hizo lulu.
Kwa hiyo, kwa urefu wa kina hicho sitozama zaidi ya hapa. Nakaribisha maoni, nasaha na changamoto zote.
Nilidadisi watu wachache kupata maono yao ili isiwe ni mimi tu naikandamizia hii nyimbo kupita kiasi..
Mshafti
Baada ya Kool Koorkichwa wa Hip Hop toka kitongoji cha Bronx jiji la New York, Marekani, na  alikuwa ana haya ya kusema:
“It’s a nice track, flows are fresh and tight, music well constructed, hook is nice too! Fiyah!”
Nimezungumza na watu kadhaa kupata rai zao. Dada Sheila Ndila wa Audio Kusini kule Kenya anasema hivi: “They did justice to the beat, they killed it already…hai-need refix, ishamalizwa.”
Gumzo letu na Buddha Blazemuandaaji wa matamasha kama WAPI ya kule Nairobi na mwandishi mahiri wa gazeti la zamani la Phat, lilipelekea yeye kudondosha ujumbe huu: “@Rhymson Tanzanian MCs do have the baddest style in Africa. They sound so flawless is like they born for hip hop. Their flow is the illest.”
Kuna shabiki mwingine wa muziki anayeishi ughaibuni, Joyce Mategero, na maoni yake yalikuwa kama ifuatavyo: “Ushairi mkali sana, una kina haswa — na kweli Vina Mpaka Uchina. Ah nimewapenda sana. Heshima zao wabongo wanaondoka hatari.”
Wote hao wametoa miwa (kinasa sauti au maiki) mitano mitano kwa wimbo huu. Maoni ya hao ndugu hapo juu yalinisaidia kujihakikishia kuwa sikuwa nashobokea tu hawa madogo — ni kuwa Vina Mpaka Uchina ni aina ya wimbo unaoweza kukusafirisha masafa ya mbali sana. Kwa heshima na taadhima nagotea hapo.
Pamoja!

Tuesday, June 18, 2013

MASHAIRI YA SWAHILI YA MWANA HARAKATI STEREO !


chini mdundo kama kawa, vocal ya kigumu
hizi flow haziendi sawa na miondoko ya kidumu
tisha kama fever viva black, viva nature
naskika mpaka geniva, beniva deliver lecture
maisha sio matamu ujumbe huu hapa sio wa kibubu
nazijua kalamu hata kabla sijakuwa vidudu
kipaji nina ujuzi wa mengi unanifanya nisishinde bubu
wanga wakikesha mungu atanilinda nisipigwe juju
acha kasumba kayumba anayumba wema
nakusaka mchumba nikifa muumba ataniumba tena
speech kibao kumbe na masnitch nao wanadunga
unaweza ukapata mchumba, na usipate unyumba mwema
neema za manati, rehema za hayati
nnapotema sina wema, ukiwa nyangema au wa masaki
cheza kila game na usicheze bila nguo
bongoflavor kama demu yule mliyekutana chuo
mi ni mmang'ati mwenye beef na mmasai
nipe shati niko safi kama trip za makhsai
donoa touch niwamiminie mwani
ka vipi uibuke church niwafukizie ubani

yes yes yoh MIC check moja mbili
nipe dili soldier kisomi hoja jadili
kila dalili naikamilisha kamili
na pili yeah
mkongwe nawakilisha swahili

yes yes yoh MIC check moja mbili
nipe dili soldier kisomi hoja jadili
kila dalili naikamilisha kamili
kwenye boom bump rap nawakilisha swahili

nipo simple kama shaolin mocca
bench humuoni messi hii ni shaolin soccer
shaolin coca kata kiu piga mbiu
mistari inatema sumu kama shaolin nyoka
haina mbada jepesi
james teach your best teacher best preach
na bless preach the best preacher
niko busy kama daladala
kwatia ngongoti haiwatoshi nyie wafupi kama mwala
peace kwa jangala, VIP ni diss mbagala
mpagani anapokufa hatufanyi mazishi kwa sala
tawala kama tinga, wanakulinda na maadui
huwinda kama simba wapo wanaokuwinda na huwajui
chekecha ubongo balongo pepesa chongo
pendeza na shuka tembeza suka pepeza chombo
mfuate darasani amani proffessor kombe
more hewani kama ruhani aliyepoteza ng'ombe
chafua midundo kama goli ndani ya boxer
mi malenga meander lenga ninapolenga siwezi kosa
nitabaki juu, sema style ya flow
sikiliza  ngoma mbona  mbishi noma stereo song


yes yes yoh MIC check moja mbili
nipe dili soldier kisomi hoja jadili
kila dalili naikamilisha kamili
na pili yeah
mkongwe nawakilisha swahili

yes yes yoh MIC check moja mbili
nipe dili soldier kisomi hoja jadili
kila dalili naikamilisha kamili
kwenye boom bump rap nawakilisha swahili

usiishi kwa mashaka ka unavuta bangi central
nakupa tag kama chunda badi spenko
sina beto hapa ngumi tu kama mkabaji keko
piga nyeto, niite dalali ukihitaji ghetto
mi ni mentor wa mentor na mentor wako
sound inventor sipo scout na peta na gangster wako
waambie wazungu hii ni sala ya mizimu
naona malaya wanasambaza waya ka mistimu
unda timu, unda darasa nije mwalimu
mkali kama mbogo na dogo mwendawazimu
sifai nyooka divai coca nakula nyonga
sing'ai chokaa sivai mocca nakula donga
najua dada yako hapendi rap kabisa
na hii kudrop na kustop ni kuasi kanisa
verse ina sura mbaya kama nduli amini
yeah, unadhani nani mkali kama sio duli na mimi



yes yes yoh MIC check moja mbili
nipe dili soldier kisomi hoja jadili
kila dalili naikamilisha kamili
na pili yeah
mkongwe nawakilisha swahili

yes yes yoh MIC check moja mbili
nipe dili soldier kisomi hoja jadili
kila dalili naikamilisha kamili
kwenye boom bump rap nawakilisha swahili

MASHAIRI YA PROPAGANDA YA MWANA HARAKATI FID Q!


Machungu unapozimwa,ili ufunikwe na asiyeweza/
Mbaya zaidi wanampa Promo halafu kwenye Show unammeza/
hautaki kuwa tatizo sababu unaweza tatuka/hauwezi jua wapi nitatua ka Jiwe gizani likitupwa/
wanaficha ili nisione wakati tayari nishajua/hamkomi? igeni nione jinsi msamba mnaupasua/
hivi mnaishi ili mle au mnakula ili muishi?/
kumbuka a small leak will sink a ship/
mazingira hatarishi, Mabwana afya wanamaPesa Mob/
uswazi tunaomba mvua zinyeshe ili tutapishe vyoo/
ogopa kuoa haraka kama unaogopa talaka/
na ukivote in a hurry ujue unaproduce corruption/
maneno yao ni matamu lakini midomo yao inanuka/
ukipewa usisahau,ukitoa TOA bila kukumbuka/
usihofie kupitwa ilimradi muda haukuachi/
amini kesho itafika kama ipo ili uipate/
tunachukiana kwasababu tunaogopana/
tunaogopana kwa sababu hatujajuana/
hatujuani kwasababu tunatengana/
dunia ni nzuri.. walimwengu hawana maana/


(KIITIKIO)

Polisi wanasapoti Gangsta Rap ''ili uhalifu uongezeke''
Wabana pua kuimba mapenzi ''je itafanya ukimwi usepe''
Media zinapromoti beef ''wanadai zinakuza mziki''
Wadau wana wasanii wabovu ''nyie wakali mtatoka vipi?''
hizi ni PROPAGANDA.. usiulize ni nani?ni yupi?saa ngapi?ilikuaje?na nani?ili iweje?
hizi ni PROPAGANDA.. utaibiwa ukicheza blanda/yule last King of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda

Polisi huniita Mzururaji na wanajua mie ni MC/
Kisha hunipa ishara kama wanavuta uradi kwa Tasbih/
Baya lisilo nidhuru ni Jema liso na faida/
nashukuru kote nasikika napotoa haya mawaidha/
kuanzia Kata,Tarafa,Wilaya,Mikoa hadi Ngazi ya Taifa/
nikifa siachi Skendo, ninauhakika nitaacha Pengo/
kwa hivi vina hata Wakulima hujikuta wanameza Mbegu/
pia ni kama Liberation struggle machoni mwa Chegu/
ukiwa mkali ka Marco Chali.. raia watafeel tu/
wajinga ndo hufa kwa wivu sababu hawako real tu/
rafiki sio urafiki usipochanganywa na Kazi/
Mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi/
haupaswi kumuamini Muongo hata kama akiongea Ukweli/
ni Dhambi kutumia Dini kama njia ya kututapeli/
wanajiingizia kipato kwa kimvuli cha misaada/
hawatufunzi tuwe Viongozi labda Viongozi wakuwafata/
utata huja, tunapoanza kuwachunguza/
badala ya kuwafata ndipo Siri zinapovuja/
tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga/
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda/
kama umevutiwa na Asali, jiandae kumkwepa Nyuki/
hauwezi kumtisha kwa Mawe Adui aliyeshika Bunduki/
ni uchunguzi tu wa Kisayansi ambao haukufanikiwa/
kama ule wa Ng'ombe kula Nyasi tu halafu anatoa Maziwa/
(KIITIKIO)
Polisi wanasapoti Gangsta Rap ''ili uhalifu uongezeke''
Wabana pua kuimba mapenzi ''je itafanya ukimwi usepe''
Media zinapromoti beef ''wanadai zinakuza mziki''
Wadau wana wasanii wabovu ''nyie wakali mtatoka vipi?''
hizi ni PROPAGANDA.. usiulize ni nani?ni yupi?saa ngapi?ilikuaje?na nani?ili iweje?
hizi ni PROPAGANDA.. utaibiwa ukicheza blanda/yule last King of Scotland sio IDD AMIN wa Uganda

Monday, June 10, 2013

Hali ya Mandela inasemekana kuwa tete!





Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.

"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''

Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.

Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.

Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.

Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.

Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.

Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.

Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.

Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.

Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela.

Thursday, June 6, 2013

SOMA MASHAIRI YA MWANAHARAKATI One The Incredible!

Habari noko/Nina habari moko
Huwezi timiza kazi kama askar choko
Juu ya daftar ninatafakar msoto
Kwa mistar mitamu kawa cariban coco
Mi ni classic na move kama dancE
Nawapa hisia kali zaid ya muvi za mikasi
Kwenye chart zao wao ushndani mm nafasi
Sifanani nao mimi ni zao wao ni nyasi
Mwanaharakatikama kikosi na siasi
Mistari ina siri nzito kama boksi la risasi
Sipo copy npo confident conscious reaction
Kwenye boof niko lost kama part ya duratics
/Geneous nilifeli kupass Mathematics
Kama rap ni drugs mi na Habit kama addicts
Sipiti kama rabbit kwenye 8 mile
Love or hate it hard iki bet hii air tym classic
Verse balanced ka account ya fisadi
Kwako mlevi wa u star ka round za vinywaji
Dunda kavu au bounce na vinywaji
Skia biashara kwenye speaker leta sound ya miradi
Naujumbe mtam kama sound ya kingasti
Snitch hastaround niko down na illematics
Na spiti kwenye mic ka risas nipo kasi
So huwez pass around ka upo stack kwenye trafficks
Aah sibutui nashoot kasi
Tu hujui siku zote vipi unisumbue kilaza
Mdundo mweusi nausugua ka na msasa
Mpaka duke ateme slang kama movie ya kihustler
Hii kwa wote wanaoikubali sio flani na flan waipende
Mi ndo moko makutano ya mistar kama stend ya mwenge
Yafanya wengi waende mbali waache wachache wakae kizembe
Kaa mbali nasi au kaa sawa nikulenge
Sa kaa sawa snitch mi ni dawa ka Giv
Hawa wanadis lakini hawapo sawa kama sisi
Na kama mkavu hapa utanawa utakuwa mbichi
Money ni power respect 2naipata ukijua displine
Kama kiongoz wa dini nampenda mjinga na mtoaji
Mtaani wanga hunihofia kama bingwa wa uponyaji
Linda chako mjinga watu wanawinda hawako safi
Ukizingua unagongwa tako kama mznga wa konyagi
Nampenda haswa anahisi anapenda heshma
Daktar rudia darasa mimi ni ugonjwa usio na jina
Anashangaa dinner mara hawa mara huyu we ni buyu mi ni moko sawa sawa.

Wachina wakamatwa Ghana kwa uchimbaji haramu!



Ghana huzalisha kiwango kikubwa zaidi cha dhahabu barani Afrika
`Maafisa wa uhamiaji nchini Ghana wanasema kuwa polisi wamewakamata zaidi ya raia 150 wa uchina ambao wanashukiwa kuhusika na uchimbaji wa dhahabu kinyume na sheria.
Kulingana na Francis Palmdeti kutoka idara ya uhamiaji nchini Ghana,raia hao wanazuiliwa katika migodi minne tofauti nchini humo.
Mamlaka nchini Ghana ilikuwa imewataka raia wote wa kigeni kutohusika katika uchimbaji madini.
Taarifa zinasema kuwa raia wengi wa uchina wamekuwa wakihusishwa na uchimbaji madini wa kiwango cha chini nchini humo baada ya kuingia kinyume cha sheria kupitia mataifa jirani.
Hata hivyo msemaji wa ubalozi wa uchina nchini Ghana anasema kwamba anataraji kuwa raia hao watarudishwa makwao.
Wakati huohuo, wizara ya mambo ya kigeni ya Uchina imelalamikia serikali ya Ghana baada ya wafanyakazi hao wa China kuzuiliwa kufuatia msako uliofanywa wa wachimbaji haramu wa madini.
Ghana ndiyo nchi yenye kuzalisha kiwango kikubwa cha Dhahabu baada ya Afrika Kusini barani Afrika.
Huku bei ya dhahabu ikiendelea kupanda katika miaka ya hivi karibuni, sekta hiyo imekuwa ikikumbwa na wachimbaji haramu wa madini hayo ikiwemo, idadi kubwa ya wafanyakazi wa kichina inayoendelea kuongezeka.
China imesema kuwa intaka watu hao kutoteswa na kutoibiwa wakati wa msako huo.

Uingereza kuwafidia Mau Mau Kenya !



Uingereza imekubali kuwalipa fidia na kuwaomba msahama walioteswa wakati wa ukoloni wa Muingereza Kenya
Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuomba msamaha pamoja na kuwalipa fidia manusura wa harakati za ukombozi wa Uhuru wa Kenya Mau Mau.
Waliokuwa wanachama wa vuguvugu hilo waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma walizodai kutendewa na uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, anatarajiwa kutangaza kiwango cha pesa ambazo serikali ya Uingereza iko tayari kutoa kama fidia, duru zikisema kuwa huenda ikawa dola milioni 20
Zaidi ya wakenya 5,000, waliteswa baadhi wakinyanyaswa na waliokuwa wakoloni wa Uingereza.
Uingereza ilipigana vita vikali dhidi ya Mau Mau, waliokuwa wanadai ardhi na kuondoka kwa utawala wa kikoloni.
Manusura wa vita hivyo wamekuwa wakiidai Uingereza kuwalipa fidia kwa miaka mingi.
BBC ina habari kuwa bwana Hague atawaomba radhi waathiriwa wa vita vya Mau Mau, wakati akitangaza kiwango cha pesa watakazotoa kama fidia kwao.
Serikali ya Uingereza awali ilikuwa imesema kuwa madai yote ya vitedno walivyofanya wakoloni ni juu ya serikali ya Kenya tangu kuipa uhuru mwaka 1963 na kuwa kwa sasa haiwezi kutakiwa kulipa.
Lakini mwaka 2011, mahakama iliamuru kuwa, wanaodai fidia, Paulo Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara, walikuwa na haki ya kudai fidia kutoka kwa Uingereza .
Mawakili wao wanasema kuwa Nzili alihasiwa , huku Bwana Nyingi akichapwa vibaya wakati Bi Mara akiteswa kimapenzi katika kambi za mateso ambako waliokuwa wanapinga ukoloni walikuwa wakifungwa.
Baada ya uamuzi wa kesi hiyo, ilirejeshwa katika mahakama kuu ili kuamua pesa watakazolipwa na ofisi ya jumuiya ya madola.
Duru zinasema kuwa serikali ilikumbwa na wakati mgumu kupata mashahidi na stakabadhi muhimu kuweza kuelezea ukweli katika kesi hiyo.
Lakini Oktoba mwaka jana, mahakama iliamua kuwa waathiriwa waliowasilisha kesi hiyo mahakamani walikuwa na haki ya kufidiwa kwani walikuwa na kesi nzito dhidi ya serikali ya Uingereza.
Watatu hao walikuwa wamesema kuwa wangekubali wahusika wa kesi kuafikiana nje ya mahakama lakini pia walikuwa wanataka kufuata sheria kwani waliona wangepata haki katika mahakama