facebook

Tuesday, September 10, 2013

SOMA HISTORIA YA STEREO B-BOY STEREO HAPA!

STEREO a.k.a B BOY STEREO 


Genre: Hip Hop

Ni tangu pale wimbo wa “nitabaki juu” ulivyoanza kusikika kwa hadhira ya Tanzania,stereo akitumia sanaa kuonyesha yeye ni nani.Stereo alianza kufuatilia Hip Hop tangu akiwa darasa la pili, mwaka 1998. Kwa kutambua kuwa ana kipaji cha kufanya Hip Hop mara baada ya kusikia ladha ya huu mziki… hatimaye alianza kuiga kuchana mistari ya emcees wengine wa Bongo, kama vile A.Y., Professor Jay, Complex (R.I.P.), Fid Q ,Solo Thang na Hasheem Dogo Mwendawazimu mpaka ughaibuni kwa kughani nyimbo za Talib Kweli .Xzibit, Jay Z, Notorious BIG, Coolio na Nas.

 Stereo alikutana na Nikki Mbishi shule ya msingi, ambapo waliendelea na huo mchezo wa kuimba nyimbo za wasanii wengine.Stereo anadai alianza rasmi kuandika lyrics zake mwenyewe akiwa darasa la nne… pamoja na Nikki.

Akiwa anaonyesha hisia zake kwa kutumia multi-syllable rhymes akipendelea kuokota maneno ya mitaani zaidi, kwa kiasi fulani, hasa yale adimu kama ‘kucheza ndondo’, ‘komando kipensi’, ‘buti lenye uvundo’, ‘msela nondo’, n.k. , mitambao ambayo wengi wanamfananisha na One The Incredible, ambaye pia anapendelea kutumia multi-syllable rhymes.Umoja wao na Nikki Mbishi aliyefanya stereo kupata deal la M-Lab umekuwa ni tochi ya kizazi kipya cha hip hop Tanzania.

Stereo anasomea “bachelor of science in urban and regional planning” huku akiendelea kushika mic na kuiwakilisha mtaa,kwa sasa Stereo yupo chini ya Unity Entertainment kampuni inayomilikiwa na A.y mkataba aliosaini mwishoni mwa mwaka 2012.


Top 5 emcees wa stereo kutoka Bongo, na kwanini?
Professor Jay, Fid Q, Nikki Mbishi, One The Incredible na Kurasa The Page. Jamaa wana mistari na flow kali sana. Sichoki kuwasikiliza kila siku sababu mistari yao inaishi. 

MHADHARA WA HIPHOP....MHADHARA WA HIP HOP....MHADHARA WA HIPHOP!

 

Kwa wale wakazi wa Bandari ya Salama zamani kuitwa MZIZIMA Ni fursa yenu na hii si ya kukosa,lakini mtajiuliza ni nini hiki? Utamaduni huu umekuja kupeana elimu/maarifa (knowledge) hivyo hatuna budi peana chakula hiki cha akili,Sasa soma hapa chini upate maelekezo. TAREHE: 13/09/2013 MUDA: 11:00 - 1:00 JIONI WAPI: ALLIANCE FRANCAISE KIINGILIO: BURE KABISA Wadau,wakereketwa wa utamaduni huu wote mnakaribishwa siku hiyo njoo ujifunze mengi kupitia ''MHADHARA HURU'' utakaotolewa na NASH EMCEE (Maalim),bila ajizi siku hiyo atatukumbusha na kutuelezea ni nini *Machata,*Wachenguaji*Wadundishaji,*Mavunjaji*Maarifa kwa wenye vipaji,

JIFUNZE MENGI KUHUSU HIPHOP


HIPHOP umekuwa ni utamaduni au nyenzo adhimu kabisa ambao unawaunganisha watu wa aina mbalimbali hapa duniani hasa kwa wale wanaoishi katika misingi yake,kwani mbali na kuburudisha hadhira yake,umekuwa ni utamaduni wa kuyaangazia mambombali katika jamii zetu kwa jicho ang'avu lisilo na shaka na kujaribu kutoa suluhu au kuchokoa mambo mbalimbali na kuwaacha watu wakiwa katika tafakuri la kipi wakifanye baada ya kuupata ukweli kupitia HIPHOP,thibitisha hili kwa kurejelea kibao cha ''NASH MC'' Kaka Suma na vingine vingi adhimu. Kila kitu kizuri huwa na changamoto nyingi mfano.ni hili watu wanaojiita WANAHIPHOP kutojifunza zaidi na kufata misingi ya utamaduni huu,hivyo ni wajibu wetu kujifunza ukweli na undani wake,

Tuesday, September 3, 2013

Monday, September 2, 2013

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MWANA FAMILIA YA WAPOTEEN CLICK KENY WAPOTEEN!

Keny Wapoteen
FAMILIA YA WAPOTEEN CLICK ILIYOPO DAR ES SALAAM KIGOGO LUHANGA

INAFURAHA SANA SIKU YA LEO KWA KUWA MMOJA WA FAMILIA YETU ANATIMIZA MIAKA KAZAA NI #KENY WAPOTEEN

TUNA MTAKIA MAISHA MAREFU YENYE FURAHA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKE

PIA ASISAHAU KUMSHUKURU MUNGU KWA KUMFIKISHA HADI HAPA ALIPOFIKA, PAMOJA NA KUWAHESHIMU WAZAZI WAKE...!!