facebook

Tuesday, May 20, 2014

Rais Morales kucheza kiungo cha kati.



Rais Morales ni shabiki sugu wa kandanda
Hebu tafakari rais wa nchi kuchezea klabu ya kandanda inayoshiriki ligi ya taifa ya daraja la kwanza ?
Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo cha kati kuanzia Agosti mwaka huu.
Rais Morales atalipwa mshahara wa dola $213 kwa mwezi .
Morales atavalia jezi nambari 10 katika klabu hiyo iliyoko Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.
Mashabiki wanamsubiri kwa udi na uvumba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni shabiki sugu wa kandanda kushuka dimbani.
Rais huyo ambaye ni shabiki sugu wa kandanda na mwenye umri wa miaka 54 ataichezea Sports Boys, timu ilyoko kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.
Timu hiyo iliyoko katika ligi ndogo ilisema kuwa rais huyo atakuwa akicheza angaa kwa dakika 20 katika kila mchuano, hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
Rais wa klabu hiyo alisema kwamba rais huyo anapenda kandanda, na kwamba yeye hucheza vizuri.

Rais Evo Morales akiwa uwanjani
‘’Tutamtumia orodha ya michuano, kisha atachagua michuano anayotaka kushiriki,” alisema rais huyo.
Edwin Tupa, mwanasiasa kutoka katika chama cha MAS, ambacho ndicho chama tawala nchini humo, alisema kuwa ndoto ya rais huyo ya kuchezea klabu ya kiitaaluma ilikuwa imetimia.
Inasemekana kuwa rais huyo yuko sawa na ni mwenye furaha katika matarajio yake ya kucheza kandanda.
Bwana Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi iliyotambulika pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine.
Mwaka wa 2007, rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekewa Bolivia, cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa katika sehemu zenye urefu.

Sunday, May 18, 2014

Arsenal mabingwa wa FA 2014.

Wachezaji wa Arsenal wakishangilia ushindi
Timu ya Arsenal ya England imetwaa kombe la FA baada ya kubamiza Hull City kwa jumla ya magoli 3 – 2 kwenye fainali iliyofanyika katika uwanja wa Wembley siku ya jumamosi.
Katika mechi hiyo ya fainali Hull City ndio waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu wa Arsenal kwa magoli mawili ya haraka haraka yaliyofungwa ndani ya dakika 10 kipindi kwanza.
Goli la kwanza lilifungwa na James Chester dakika ya 3 huku goli la pili la Hull likifungwa katika dakika ya 7 na Curtis Davies.
Hata hivyo magoli hayo hayakuweza kudumu kwani katika dakika ya 16 Santiago Cazorla aliifungia Arsenal goli na hivyo hadi mapunziko matokeo yakawa 1 – 2.
Katika kipindi cha pili Arsenal walikuja juu na kusawazisha goli hilo katika dakika ya 80 lililofungwa na Laurent Koscielny na kuwa 2 – 2 na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike dakika 90 za kawaida kwa sare ya 2 - 2 bila kumpata bingwa.
Baadae mwamuzi wa mpambano huo Lee Probert aliongeza dakika nyingine 30 ambazo zilifanya Arsenal wajiongezee goli la tatu na la ushindi katika dakika ya 108 lililofungwa na Aaron Ramsey.
Hadi mpira unamalizika Arsenal wakawa wameifunga Hull City kwa jumla ya magoli 3 -2
Gunners ilishinda taji lake la mwisho mwaka 2005 katika fainali za kombe la F.A ambapo iliwacharaza wapinzani wao wa jadi Manchester United katika mechi iliochezewa katika uwanja wa Cardiff,huku timu ya Hull City ikishiriki kwa mara ya kwanza katika fainali ya kombe hilo.
Meneja Arsene Wenger ameshinda mataji saba muhimu katika miaka yake 18 kama mkufunzi wa timu ya Arsenal, ikiwemo mataji matatu ya ligi kuu ya uingereza pamoja na manne ya kombe la F.A.
Mashabiki wa timu zote mbili walikabidhiwa tiketi 25,000 kila mmoja huku tiketi nyengine 20,000 zikipewa watu waliojitolea katika mashirika ya hisani,vilabu na ligi za kaunti.

5 wauawa katika mlipuko Nigeria.

Mlipuko wa bomu Nigeria
Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.

Mashambulio ya awali

Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.

Monday, May 12, 2014

Boko H: Waonyesha wasichana waliotekwa.

Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

Friday, May 9, 2014

Riadha ya Diamond League kuanza leo Doha.

Usain Bolt anayetarajiwa kushiriki riadha ya Diamond League itakayokuwa Doha, Qatar.
Ni Mashindano ya Riadha yanayopambwa na wakimbiaji nyota duniani na huu ni mkondo wa kwanza.
Kuna jumla ya mikondo 14 ya mbio hizi ambazo zitamalizika tarehe tano Septemba mwaka huu mjini Brussels, Ubelgiji.
Mabingwa kama vile Usain Bolt , Yohan Blake huwa vivutio vikubwa lakini muhimu zaidi mashindano hayo ni jukwaa mojawapo kubwa la kuonyesha nyota wa Afrika mashariki na kati.
Miongoni mwa wanaotarajiwa kupeperusha bendera ya Afrika kama kawaida ni wa-Ethiopia kama vile Mohamed Aman na wakenya , akina Job Kinyor, Kipkorir Mutahi wanatarajiwa kumpa upinzani mkali Nijel Amos mshindi wa medali ya fedha mbio mita 800 katika olympiki iliyopita ya London kwani bingwa David Rudisha mkenya huenda asishiriki kwa sababu angali anauguza jeraha.
Katika mbio kama zile za mita 3000 kuruka viunzi, wake kwa waume wakenya hufanya vizuri lakini ushindani ni mkubwa.

Thursday, May 8, 2014

USAIN BOLT ASAKA VIATU VYAKE.

Viatu vya Bolt vinagharimu pauni elfu 20 hizo ni dola elfu 34 za kimarekani
Mwanariadha Usain Bolt hana raha, anatafuta viatu vyake vilivyoibwa.
Mwanariadha huyo bingwa wa Olympic wa mbio fupi sasa ameeingia kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa twitter ulio na zaidi ya mashabiki millioni 3 wanaomfuatilia, akisihi 'jamani najua si tumarafiiki.., aliyeonea viatu vyangu au aliyenavyo tafadhali uvirudishe'!
Viatu hivyo vya michezo rangi ya chungwa chapa cha Puma ,alivyowiweka saini yake vinagharimu pauni za Uingereza elfu ishirini.
Majajusi wa Scotland Yard wanasema viliibwa wiki iliyopia mtaa wa Craydon huko London maeneo ya viwandani vilipokuwa vimeekwa kama maonyesho.
Pia nao wanasihi atakaekuwa na fununu yoyote kuvihusu apige ripoti polisi.
Picha za viatu hivyo alivyovaa Usain alipotwaa ushindi zimezagaa mitandaoni, na sasa anaweka saini pair nyengine atakayoipelekea huko Uingereza.
Wadadisi wanasema itabidi ulinzi wa viatu hivyo uimarishwe zaidi.

Wednesday, May 7, 2014

Mvua ya Samaki Sri Lanka.

Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali
Wakaazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo.
Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.
Wanakijiji hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu kizito kikianguka na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa
Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.
Wakazi wanasema sio mara ya kwanza kwa mvua ya Samaki kuwanyeshea
Viumbe hawa wa majini wanaweza wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa kushikiliwa na mawingu hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha.
Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.
Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo badaye.
Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.
Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi wa Marekani na Uingereza.
Samaki wamadhamana kuu Sri Lanka.

Tuesday, May 6, 2014

MASHAIRI YA SHABIKI BY MANSU LI.

MANSU LI.

what is it now
what is it now

Ubeti1:
Nilimuona shabiki tu ambaye ananikubali
na wala sikutaraji angeweza kufika mbali
mara miezi inapita tunajuana kiundani
Shabiki akawa rafiki anakuja mpaka nyumbani
Siri moyoni sielewi ana nia gani
mara akinikosa hewani kwake tafrani
kumbe shabiki alisha-fall in love
lakini ni too late men, oh my God
Anasema hawezi bila mimi
nilishamteka akili na hajui afanye nini
huku nae mamaa anahisi namzunguka
sio mimi wa zamani anadai na-change hulka
Shabiki gani anayepiga hata usiku
ukiuliza kwanini anasema i miss u
kwanini mamaa asipoteze amani
na huku anajua fika hili penzi limashakani

(kiitikio)
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that

Ubeti2:
Anadai mara ya kwanza aliniona kwenye tv
kwenye video ya KINA KIREFU long T
kisha akaniona kwenye TUKO PAMOJA
na hapo ndipo akachoka kungoja
Siku ya siku ilikuwa kwenye show
akajikaza kisabuni pasina kuona soo
excuse me,inakuaje bro?
sio siri nimependa vile unavyo-flow
Nikasema asante kisha tukaachana
kumbe haikuwa mwisho baada ya kuagana
sijui ni wapi alipopata yangu namba
ndivyo hivyo akaanza kuniganda
Anataka tuchat saa zote
anasema ni mimi naemuondoa upweke
hata kama ninae anasema, i don't care
mazoea yana tabu na yeye alishanizoea

(kiitikio)
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that

ubeti3:
You’re so cute
But I can’t be with you
sitaki kukuchezea halafu nikipe kitu
Maybe just a friendship kama kwako sio ishu
Please understand me I’ll never be with you
Sikujua ukweli unaosema ungezusha vita
Sms za matusi zikaanza miminika
Akunielewa alihisi tu naringa
Bora lawama acha anione mjinga
I keep gangster girl I keep it real
Am so sorry I can imagine how you feel
Vipi utajiskia nikiku nikakuacha
Am not a player am street hustler
Inataka moyo kuwa kioo cha jamii
Sometimes tunateleza sisi sio manabii
Hapa ndipo wengeni uzalendo unapowashinda
Na isiwe tabu basi wanafanya kibingwa

(kiitikio)
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that

MASHAIRI YA KIPIMO CHA PENZI AZMA FT KITA!


INTRO
ah ah ah aha ha ah EI ZED EM EI(AZMA) ah ah aha yo yo



VERSE I (AZMA)
Kila men anakuaproach, anataka mikasi,hujui cha kufanya,
Bora umurike kaa unatochi, ujue kipimo ni hasi ,au kipimo ni chanya,
Kama kipimo ni sex,mbona mmefanya wee, na bado mchizi akakuacha,
Kama dereva wa teksi,mbona umesanya wee, waka peez wakakuacha.
Kama love ni glass,basi tugonge chears,
Kama love ni class,basi tufute tears,
Ulishawahi kuwa na mpenzi,akakuacha solemba,
Akakugeuza kama mshenzi,ukavikwa kiremba,
Ukajuiuliza whats wrong, au sijui kupenda?
Unapaswa kuwa strong,japo walishakutenda,
Hakuna love chini ya jua,usiingie kichwa kichwa,
Ni bora leo uka jua,usiishie fichwa fichwa.
Mapenzi yamegeuka fimbo,wengi hatujui kutenda,
Uongofu umegeuka wimbo,wengi hatujui kupenda,
Anayekupenda kisa mwanya,uking’oa itakuwaje?
Anayekupenda unavyofanya ukimuoa itakuwaje?.
yeh u better think twice ah ha ha MUJWAHUKI.


CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue

VERSE II AZMA
Je kipimo ni mita,au ni sentimita?
Je kipimo ni lita,au ni senti lita?
Aliyekupenda kwenye shida,itakuwaje kwenye rahaa?
Pasipo love ni kawaida,kuna kuachwa kwa mataa,
Walioana mchana,usiku wakatengana,
Walipendana kwa sana,hawakuweza kulindana,
Kama kipimo ni imani,wengi walishaaminiana na mwisho wakafumaniana,
Kama kipimo ni amani,wengi walisha ridhiana na mwisho wakatalikiana.
mpenzi anapozembea, ndio mwingine anapokata hamu,
Aanapenda unavyotembea, au anapenda unavyotabasamu,
Mnagombana kisa shory,anayemegwa kila dakika,
Mapenzi yamegeuka story,na hadithi za kusadikika,
Mliokutana kwenye baa,mnaoana kwenye gesti,
Mnainuka na kukaa,mlioshindwa kwenye testi,
Aliyeachana na mkewe,amemuoa house girl,
Usiombe ukawa ni wewe,unayegeuzwa tom and jelly,
Anayekupenda unamkataa, we unapenda kwingine,
Unayemuwaza kila saa, ye anamuwaza mwingine.

CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue

VERSE III (AZMA)
Wanakupenda kisura,ama kisa mavazi,
Mapenzi sio chakula,usifiche maradhi,
Mwanzo washakutapeli,ukabaki umesizi,
Wanakupenda kiukweli,hiyo bado ndio quiz,
Inakuwaje kama una mpenzi,mmeshamaliza sex,anataka umlipe,
Utajuaje kama kuna penzi,huduma imegeuka tex,upande na ulipe,
Kama kipimo ni mtoto,mbona umeshazalishwa na jamaa akasepa?
Kujua kipimo ni ndoto,uongo umeshahalalishwa wanakomaa na paper. love in epa, they love ur paper,
utapay price ukidata na foreign love,think twice before hujafall in love
kama kipimo ni tabia,mbona binti malkia,kaolewa n a muuza gongo?
Waliokutana kwenye bia,leo washanitamkia,penzi lao sio la uongo.
Kuna ulimbo,kwani urembo,umegeuzwa biashara,
Kutoka chimbo,we ni gembo,unanasa kwa ishala,
Wangapi ushawadanganya,eti usiku haujalala?
Wangapi ushawachanganya,haya mapenzi ni jalala?

CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue

Tahadhari kwa wezi wa simu mitaani!

Mwizi aliyepigwa picha na simu hiyo ya HTC
Simu ya mkononi iliyokuwa imeibwa, ilituma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha kuwa ndiye mmiliki wake.
Polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo.
Simu hiyo aina ya HTC, iliibwa kutoka kwa koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.
Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza nambari ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.
Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanamume huyo alipojaribu kuingiza nambari hiyo bila kufanikiwa.
Barua pepe ya mwanafunzi huyo ilituma ujumbe kwa polisi kuwaarifu kuhusu wizi huo.

Friday, May 2, 2014

AZMA MUNGU INUSURU TANZANIA OFFICIAL VIDEO.

P THE MC & SONGA HUNA JIPYA!

         

VIDEO YA RADO USIULIZE

Aliyemtupia Ndizi Alves akamatwa.


Alves alikula Ndizi aliyotupiwa akisema vitendo vya kibaguzi vimekithiri katika soka Ulaya
Polisi nchini Uhispania, wanasema wamemkamata shabiki aliyemtupia mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya Jumapili akiwa uwanjani.
Dani ni raia wa Brazil anayesakatia soka yake katika klabu ya Barcelona.
Kitendo hicho cha ubaguzi kilitokea wakati Alves alipokuwa anajiandaa kupiga mpira wa kona uwanjani siku ya Jumapili.
Alves alichukua Ndizi hiyo na kuila, kitendo ambacho kimemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii.
Shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.
Alves amesema kuwa amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi kwa miaka sita
Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha.
Mchezaji huyo alisema alishangazwa sana na uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono Alves.
Barcelona walishinda Villareal mabao 3-2 katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa El Madrigal mjini Castellon pwani ya Hispania.
Alves aliambia BBC kuwa kilichomkumba sio jambo geni, na kwamba amekuwa akipinga vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa miaka sita.