facebook

Monday, June 30, 2014

Hip Hop Ya Tanzania: Ni ubunifu au kubuni tu.

Chimbuko la Hip hop linaweza kufafanuliwa kwa kifupi kama ‘juhudi za wasiojiweza’. Hili lilionekana dhahiri wakati Wamarekani weusi walipokuwa wakipigania haki zao za kijamii, wakati huo wa civil rights movement. Hapa kwa haraka tunaona uhusiano wa Hip Hop na jamii. Hip Hop ikiwa upande wa wanyonge, ikitumika kama sauti ya wakandamizwaji.
Miaka hiyo imekwishapita na muziki huu umekua na kuwa ni utamaduni. Lakini bado umebaki na damu ya uanaharakati. Hip Hop imebadilika kama tamaduni yeyote ile, na mpaka kuvuka mipaka. Mipaka hiyo ilivuka hadi kufika Tanzania ambako ilikaribishwa. Boardman anajenga hoja kuwa, Hip Hop ilifanikiwa kuvuka mipaka ya Tanzania kutokana na kuanguka kwa Siasa ya Ujamaa. Mwanzo ulikuwa mgumu, na bado safari ni ndefu, lakini mafanikio yanaonekana; kama kukubalika na jamii.
Muziki huu hata hivyo bado unaonekana kama ni tamaduni ya Kimarekani zaidi, huku kuna baadhi ya watu kwenye jamii zetu ambao wanaona Hip Hop ya nyumbani ‘ina-recycle’ tu yale yanayofanywa na wasanii wa Marekani. Kwenye hilo natumaini kuwa kila mtu atakuwa na mawazo yake, lakini ili kupata jibu lililo karibu na sahihi, ni vizuri kurudi kwenye chimbuko la tamaduni wa muziki huu wa Hip Hop.
Muziki huu ulikuwa unaitwa “muziki wa kufokafoka” kipindi hicho. Nadhani hilo jina halikuwa sahihi, na uliupa mziki huu taswira mbaya. Lakini kwa kuwa ulikuwa ni muziki mpya, inawezekana hatukujua jina gani litakuwa sahihi. Hata hivyo, ukiangalia kwa karibu labda neno kufoka halikukosea sana, kwani kurap ni kama kufoka — lakini neno sahihi la Kiswahili ni kughani.
Muziki huu ulileta mgongano kati ya kizazi chetu na kizazi cha Tabora Jazz kwani muziki huu uliangaliwa kwa tafsiri tofauti. Muziki huu ulionekana ukiwa na hiyo dhana ya kufokafoka, na kawaida ya tamaduni zetu, mtoto hamfokei mzazi. Hivyo inawezekana Hip Hop ikaonekana ni muziki unaochochea uasi dhihi ya tamaduni zetu za ndio mzee. Lakini kwa upande mwingine, hasa ukiangalia katika chimbuko, huu ni muziki wa watu wanaokandamizwa. Hivyo kipindi kile cha akina II Proud na Wapi Tunakwenda, vijana tulikuwa na madukuduku mengi.
Hip Hop ikafanya vile vile kama ilichofanya Marekani kipindi cha miaka ya sitini na sabini — kuwapa wanyonge sauti. Tofauti ilikuwa, huko Marekani iliwapa watu weusi (hasa vijana) sauti dhidi ya ubaguzi wa rangi. Hapa Tanzania, suala halikuwa ubaguzi wa rangi, lakini kupigania haki za vijana, dhidi ya uonevu wa polisi, dhidi ya maisha magumu kwa vijana n.k. Hivyo ni kweli, mwanzoni kwenye hip hop watu walikuwa wanafoka vilivyo, kwani matatizo yalikuwa mengi na hakuna aliyewasilisha matatizo hayo ya vijana, au hata kuyapa nafasi ya kusikilizwa. Hilo linafanana na makundi kamaN.W.A. huko Marekani. N.W.A walikuwa wakali, kwani hali halisi yao ilikuwa ni ngumu sana kipindi hicho, ukilinganisha na sasa.
Sasa kama tamaduni nyingine, Hip Hop imekuwa inakwenda na wakati, pamoja na kuwa kwenda na wakati huko hakujasaidia sanaa hii moja kwa moja. Maisha yamebadilika, vijana wa juzi waliokuwa wanapigania haki zao, leo baadhi wamefanikiwa. Hivyo maudhui ya mashairi yamebadilika kwa namna moja au nyingine. Kama marekani, vijana wengi wametajirika kupitia mgongoc wa Hip Hop, hivyo kuanza kughani kuhusu utajiri wao, kwasababu hawaishi tena kwenyeghettos kama awali.
Hapa Tanzania, kwenye nchi masikini, Hip Hop imekuwa bado ikitegemewa katika kutetea haki za wanyonge na kuzungumzia matatizo ambayo yanaendelea kukabili vijana wengi. Pamoja wapo wachache, waliofanikiwa, wengi wa vijana bado wapo kwenye hali ngumu. Hapa ndipo neno “Hali Halisi” linapoingia katika kuchambua Hip Hop ya Tanzania. Wapo ambao wanahesabiwa kama si wana Hip Hop, kwani mashairi yao hayazungumzii hali halisi ya maisha ya kijana wa kila siku wa Kitanzania. Hili linaendana na picha zilizomo kwenye video nyimbo zao. Video nyingi zinaonekana kushindwa kuakisi yaliyomo katika tamaduni zetu, bali huakisi zaidi yaliyomo katika mila na desturi za tamaduni za Magharibi.
Hili suala la mila na desturi ni mjadala mwingine, kwani video hizi huonekana kama zinakiuka maadili ya mila na desturi zetu. Mengi yamezungumzwa, bila kufafanua nini maana ya mila na desturi zetu, kwani kama suala ni mavazi ya uchi,basi kuna Wamasai ambao hutembea wamevaa lubega tu, bila kuwa na mavazi ya ndani. Wapo wengine ambao wanaona picha za kwenye video za Hip Hop zinahamasisha maovu; kwa mfano ngono, kama vile video nyingi za Hip Hop za Marekani. Kama hilo ni tatizo, basi tunaweza kubadilishakituo cha runinga na kuweka mduara, ambao naamini ni tamaduni yetu.

Robben amekiri kujiangusha

Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti
Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti ya ushindi lakini akasema alikuwa ametegwa .
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .
Robben alikunguwa katika eneo la lango Uholanzi ilipokuwa imesawazisha bao moja kwa moja na ikaisaidia Uholanzi kuibuka mshindi kwa mabao 2-1 .Herrera amesema kuwa Penalti hiyo dakika tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo haikufaa''hiyo ni njama ya FIFA kuiondoa Mexico kwenye kinyang'anyiro hicho .
Penalti hiyo ilifungwa na Jan-Klaas Huntelaar
Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti
“nataka kwanza kuwaomba radhi mashabiki wangu kwa kudanganya na kujiangusha ukweli haikufaa '' Robben aliiambia runinga ya Uholanzi NOS.
''nafikiri kuwa refarii Proenca alifanya kweli kuashiria penalti akisema kuwa alikuwa ametegwa na nahodha wa Mexico Rafael Marquez.
Mexico ilikuwa imeongoza hadi dakika ya 88 ya kipindi cha pili kabla Wesley Sneijder kuisawazishia Uholanzi kabla ya Huntelaar kufunga penalti iliyozua ubishi mkubwa.
Herrera alisema kuwa haikufaa refarii kutoka ulaya alipewa mechi kati ya timu kutoka ulaya na Marekani ya kusini.

Kwanini FIFA hawakutupa refarii mwafrika mhindi ama hata refarii kutoka Marekani kusini ?

Thursday, June 26, 2014

Obama aomba pesa awasaidie waasi.

Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.
Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.

Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.

Monday, June 16, 2014

Mwanamziki apasuliwa huku akiimba.

Alama Kante afanyiwa upasuaji
Katika tukio la kwanza la aina yake mwanamziki mmoja nchini Ufarasa amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba.
Madaktari wanasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.
Mwimbaji huyo Alama Kante, ambaye ni raia wa Guinea anayeishi Ufaransa alipewa dawa za kumfanya asihisi uchungu wakati upasuaji huo ukiendelea.
Kante alikua na hofu kuhusu kupoteza sauti yake kutokana na upasuaji huo lakini daktari wake akapendekeza aimbe huku akipasuliwa ikiwa ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuwahi kuchukuliwa kote duniani.
Profesa Giles Dhonneur, aliyeongoza upasuaji huo katika hospitali ya Henri Mondor hospital, ameonyesha video ya mwanamziki huyo akiimba huku naye akiendelea na upasuaji. Ameelezea matuamani kuwa mambo yatakuwa sawa.
Amesema ni uchungu sana kufanya upasuaji kama huo bila kutumia dawa ya kumfanya mgonjwa asihisi uchungu lakini mbinu na dawa aliyotumia ilimuwezesha Kante kuhimili bila matatizo yoyote.
Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao.

Ufaransa yafaidi teknolojia ya goal.

Ufaransa yafaidi Teknolojia ya kuwasaidia marefarii Brazil 2014
Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufaidi matumizi ya teknolojia ya kisasa kuzuia ubishi katika mechi ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.
Karim Benzema alikuwa anatekeleza mashambulizi katika lango la Honduras kunaklo dakika ya 48 ya kipindi cha pili lakini kipa wa Honduras Noel Valladares akababaika na mpira ukavuka laini kisha akaunyofoa mara moja na

kukimbia akitaka kuupiga kama 'goal kick' lakini mpiga kipenga kutoka Brazil Sandro Meira Ricci akapuliza kipenga na kuashiria bao kutokana na mtikiso kwenye saa yake inayoambatana na teknolojia hiyo ya kisasa ya goal line.
Mashabiki na wachezaji wa Honduras waliokuwa ndani ya uwanja wa Porto Alegre walijaribu kupinga kauli ya refarii huyo lakini wapi alihakiki bao hilo la pili usiku huu kwa Ufaransa .
Honduras ilikuwa tayari imempoteza mchezaji wao Palacios mwisho wa kipindi cha kwanza alipoonyeshwa kadi ya pili ya manjano
Teknolojia hiyo inayotumika kwa mara ya kwanza inajumuisha kamera 14 za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa kurekodi picha na sauti kwa kasi mno na mpira ambao inasambaza
Ufaransa yafaidi Teknolojia ya goaline dhidi ya Honduras Brazil 2014
Kamera hizo zinauwezo wa kuchukua picha kwa kasi mno (saba kwenye kila lango), katika paa za nyanja zote 12, Brazili.
Kamera hizi zimeunganishwa kwenye tarakilishi inayounda maumbo na kuondoa umbo lolote lile ambalo sio la mpira, kisha kufuata mwenendo wa mpira kwa kadri milimita chache, kampuni hiyo ilisema.
Mpira unapovuka tu mstari wa lango, utakuwa unapeperusha ujumbe kwenye saa yake mwamuzi wa mechi, kisha ujumbe wenye maandishi ‘GOAL’ unatokea kwenye saa hiyo pamoja na mtikisiko (Vibration).
Haya yote yanafanyika kwa muda wa chini ya sekunde moja.
Ufaransa yafaidi Teknolojia ya goaline dhidi ya Honduras Brazil 2014
Mfumo huo ambao tayari ushajaribiwa na Fifa, katika kombe la Mashirika mwaka uliopita.
Kampuni ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa, ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya michezo.
Hii itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa katika mfumo wa kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High Definition (UHD), ujulikanao kama 4K Format, ambayo kiwango chake ni mara nne zaidi ya kiwango cha
televisheni za kawaida.
Teknolojia yamsaidia refarii kuipa Ufaransa bao
Hata ingawa suluhisho hii imetumiwa kwa miaka mingi katika michezo mingine,kama Tennis Cricketi na Raga hii itakua mara ya kwanza teknolojia ya lango la goli kutumika katika kombe la dunia .
Ni mfano mmoja tu wa jinsi kombe hili la dunia litakavyokua lenye teknolojia kubwa zaidi na lenye kujumuisha miundo mbinu ya teknolojia ya karne ya 21.