Kifo cha Mwanafunzi wa Chuo kikuu nchini Kenya kimezuaa shutuma mpya za mauaji yanayodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi nchini humo.
Ripoti zinasema Evans Njoroge, mwanafunzi ambaye alikua kiongozi Chuo kikuu cha Meru nchini humo, aliuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa polisi.
Mwandishi wa BBC, Ferdinand Omondi anasema pichaza mwili wa kijana huyo, damu yake ikionekana imetapakaa kote, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku raia wa Kenya wakighadhabishwa na kile walichodai kuwa mauaji yanayotekelezwa na polisi.
Evans alipigwa risasi Jumanne wakati wa maandamano ya wanafunzi waliokuwa wakilalamikia ongezeko la ada dhidi ya chuo cha Meru.