Tamadunimuzik.....Yeah
Combination sounds....
Combinenga.....
Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2
Verse 1:Nikki Mbishi
Vaa wema vua shari safari hatua,
Round hii mbishi niko gengeni na jua kali,
Siuzi nyanya vitunguu wala pilipili hoho,
Too little too late ushachelewa Jojo,
Wakiniona mi nashine wanachonga,
Ndo maana kila line wanaponda,
Vipi nikisign na Anaconda,
Busy kwenye show mi nashow biz na kwa flow hizi si ndo time ya kusonga,
Hahahahaaa!!! hii ni hit ya kubaki,
Mwenyei kaniumba fit ndo maana lift sitaki,
Nabang kila session mpaka morning groove,
Eti niko chini hunioni juu?,Mi ni leader wa performing crew,
Nizungue ubaki mweupe design ya hair style ya Monikuu,
Haah Nikki Mbishi Songa One The Incredible,
Komando Yosso ni mzozo ngoma ni terrible,
Karibuni..
Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2
Verse 2:One the inredible
Wanasema wanapenda vile mi hubonga kila kitu,
Rap sonara madini huwa nachonga kila siku,
Sina fleva za kibongo naonja kila kitu,
Bila woga wanaloga niwe kioja kila siku,
Kama unaipenda push play ama itose,
Everyday iwe kush nei ama okayyy,
Wazushi msichoke naghushi ninyooshe,
Nipe changamoto sio kila nikigusa tu okayyy
Kuna watu wangependa nigote kwenye misele,
Iwe kwere kote Moko nisote nisiende mbele,
Nichoke niwe kero kokote au niende selo nisitoke,
Ila msiogope nipo milele,
Kwani muumba ndo mpaji kutunga kipaji,
Niko macho wanataka kuniua niwe mtaji,
Niko Anaconda na hii ndo ile siku niko mcaho,
Ila wengi watakesha kila siku..
Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2
Verse 3:Songa
Chungu kichungu natema sumu kisumu,
Hali ni mgumu je utabeba dumu kidumu,
Na kidumu mpaka wasaa utapotambaa,
Na kushangaa kwamba kufika humu ni ngumu,
Ukicheck chance hola,unawaza utaishi vipi endapo majambazi wakipora,
Basi bora,kuwa na wasi kama polisi ni sawa na wazazi wenye bastola,
Heeey.. na bado utakosa njozi,kazi hakuna utanuna utashona gozi,
Niite Songa endapo utakosa pozi,
Au nyong'onyea zaidi ya mgonjwa aliyekosa dozi,
We si kiongozi...ndio,
Mbona maji hakuna wananchi mtaani wanaoga chozi....
(kicheko]
Chorus:JD
Siku ikifika tukubali,tuwe macho
Kupanda na kushuka zote hali,tuwe macho x2
Friday, November 21, 2014
Wednesday, November 19, 2014
Familia ya Bob Marley kuuza bidhaa za Bangi.
![]() |
FAMILIA YA BOB MARLEY. |
Familia
ya aliyekuwa mwanamuziki wa Jamaica, Bob Marley imezindua kampuni
ambayo wanaitaja kama ya kwanza duniani kuuza bidhaa za Canbbisa au
marujuana au Bangi kama wanavyoijua wengi.
Bidhaa hizo
zitajulikama kama 'Marley Natural' na na zitajumuisha mafuta ya urembo
pamoja na manukato mengine ya wanawake na bidhaa nyinginezo. Bidhaa hizo zitatengezwa na kampuni kubwa ijulikanano Privateer Holdings iliyo mjini Washington Marekani, ikisisitiza kutaka kudumisha kumbukumbu ya mwanamuziki huyo aliyesifika kote duniani.
Bidhaa hizo zitauzwa nchini Marekani na kwingineko duniani kunzia mwaka jana.
Mwanawe Bob Marley, Cedella Marley, alisema hayati babake angekuwa hai angefurahishwa sana na wazo hilo.
Mkuu wa kampuni hiyo, Brendan Kennedy alisema Marley alikuwa mtu ambaye kwa njia nyingi alisaidia kuanzisha harakati za kupinga juhudi za kuharamisha Bangi miaka 50 iliyopita.
"Marley alipenda sana kutumia Bangi na hakuna aliyemshinda kwa hilo duniani kote. ''
Bob Marley alifariki mwezi Mei mwaka 1981, kutokana na Saratani.Alipenda sana kutumia Bangi kama sehemu ya imani yake ya Rastafarian na kuunga mkono kuhalalishwa kwake.
Matumizi ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika majimbo ya Colorado na Washington nchini Marekani.
Majimbo mengine huenda yakaidhinisha matumizi ya Bangi nchini Marekani na mengine tayari yanaruhusu utumiaji wa bidhaa hiyo kwa sababu za matibabu.
ONE THE INCREDIBLE KUZINDUA ALBUM YAKE MPYA, REPRESENTING AFRICA POPOTE (R.A.P) DECEMBER 5.
ONE THE INCREDIBLE KUZINDUA ALBUM YAKE MPYA ITAKAYO ITWA REPRESENTING AFRICA POPOTE (R.A.P) DECEMBER 5 KATIKA VIWANJA VYA POSTA.
PAKUA NA KUSIKILIZA WIMBO MPYA JCB ft. Hisia "Mtoto Mkali/Ghetto Love"
Bofya HAPA https://mkito.com/s…/mtoto-mkali-ghetto-love-feat-hisia/3339
Kupata wimbo mpya wa "JCB ft Hisia, wimbo unakwenda kwa jina la Mtoto Mkali/Ghetto Love"
ikiwa ni mkono wa HipHop toka Watengwa Recs Kijenge kazi ya producer Daz
Knowledge/DabRecs/Defxtro, kwa mahojiano/mawasiliano zaidi check na JCB
kwa whatsapp +45 52 750 060 pia follow @mkitodotcom @jcbwatengwa
@daznaledge @noizmekah @hisiatz powered by @vmgafrica www.vmgafrica.com #supportafricanartists #shidampya #YKMK
BEEF KUTOKA KWA SONGA IJUMAA HII.
KWA UPENDO WENU MLIOONESHA WIMBO UTATOKA IJUMAA HII,UNAITWA "BEEF."
LIKE,COMMENT,SHARE NA ITAKUWA POA ZAIDI KAMA UTAIWEKA HII PICHA KAMA PROFILE PICTURE YAKO.
S/o KWA KUMKICHWA KWA COVER ART.
#Songa
#Beef
#ThisFriday
#StayTuned
Thursday, October 9, 2014
NASHEMCEE TEMEKE SHOW ZIME BAKI SIKU 9 TU.

kama bado hujapata tiketi yako ya mapema kwa 3000/= unaweza kupiga namba 0769 522 346,0656 769 665
Kwa washkaji wa kiwalani,na Vingunguti cheki na P The-mc Polymath 0717 254 451 au 0713 492 216...kumbuka mlangoni itakua 4000/=
Tuesday, September 16, 2014
Thursday, August 21, 2014
Fid Q aifafanisha ‘Bongo Hiphop’ na msichana anayempenda kwa dhati kwenye wimbo mpya.
Kwa mujibu Fareed Kubanda aka Fid Q, ‘Bongo Hiphop’ ni msichana
anayempenda kwa dhati na wataishi pamoja katika shida na raha. Fid
ameonesha msimamo huo kwenye wimbo wake mpya ‘Bongo Hiphop’ aliouchia
kwenye siku yake ya kuzaliwa (August 13) na kumshirikisha producer
mkongwe, P-Funk Majani.
Kwenye wimbo huo, Ngosha anaelezea jinsi ambavyo hiphop ya Tanzania
ilianza kabla ya Bongo Flava japo wasanii wa hiphop wengi hawafaidiki
kiuchumi ukilinganisha na wasanii wanaoimba.
“Bongo Flava mzuri kiasi hiphop wewe ndio my queen, my first, my
last and everything in between,” anarap Fid. “Kama kukupenda wewe ni
dhambi basi shetani yu nami, na kamwe sitonyea kambini ili niwabambe
dukani,” anasikika rapper huyo.
Pamoja na wimbo huo, Fid pia ataachia documentary yenye jina hilo
(Bongo Hiphop) ambayo itazungumzia historia ya muziki wa hiphop nchini.
Mfahamu Jyoti, mwanamke mfupi zaidi duniani 'Sentimita 60' anaepata deals kubwa Marekani.

Jyoti Amge, mwenye umri wa miaka 21, ndiye mwanamke mwenye kimo kifupi zaidi duniani akiwa na urefu wa inches 24 (sawa na urefu wa rula mbili za sentimita 32).
Jyoti ambaye ni mkazi wa Napur, India, aliingia rasmi katika kitabu cha Guinness mwaka 2011 kama mwanamke mfupi zaidi duniani aliye hai na tayari ameshapata deals kubwa kwa kimo chake.
Amewahi kushiriki katika makala maalum ya Body Shock: Two Foot High Teen na August 13, na mwaka huu alipata deal ya kuigiza katika ‘American Horror Story: Freak Show’.
Mwanamke huyo ambaye kimo chake kinatajwa kuwa kimetokana na tatizo la kutokua kawaida ‘achondroplasia’ anaendelea kupiga deals kubwa na amegeuka kuwa lulu kwa muonekano huo wa kipekee.

Jyoti akiwa amebebwa
Rais wa Colombia aunga mkono Bhangi.

Rais wa Colombia aunga mkono kuhalalishwa kwa Bhangi
Rais wa Colombian Juan Manuel Santos amesema kuwa anaunga mkono matumizi ya bangi kwa minajili ya utabibu.
Bwana Santos ameunga mkono mswada ambao utapigiwa kura bungeni wakati wowote kwa manufaa ya kupunguza uchungu kwa wagonjwa .
Rais wa Colombia aunga mkono kuhalalishwa kwa Bhangi
Colombia ni moja kati ya mataifa ambayo yamekumbwa na vita vya walanguzi wa madawa ya kulevya na serikali vita ambavyo vimesababisha mauaji ya mamia ya watu. .
Marijuana inakuzwa kwa wingi nchini Colombia, lakini taifa hilo linajulikana kote duniani kwa ukuaji wa cocaine, kwa pamoja na Peru.

Bhangi inakuzwa kwa wingi nchini Colombia
"natumai tutaliangazia jambo hili la matumizi ya marijuana kwa mtazamo mpya utakaofaidi wagonjwa ambao wanaitegemea kupunguza uchungu.'' alisema bwa Santos akiwa mjini Bogota.
Friday, August 15, 2014
Picha: Adidas na FIFA wamkabidhi James Rodriguez mzigo wa dhahabu.
Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limekabidhi tuzo ya
mfungaji bora wa fainali za kombe la dunia zilizohitimishwa nchini
Brazil July 13 mwaka huu, mshambuliaji kutoka nchini Colombia na klabu
ya Real Madrid James David Rodríguez Rubio.
FIFA wamemkabidhi tuzo hiyo Rudriguez mwenye umri wa miaka 23, ambayo ni kiatu cha dhahabu mjini Madrid ikiwa ni sehemu ya kutimiza makabidhiano ya zawadi kwa washindi mbali mbali wa fainali wa kombe la dunia za mwaka 2014.
Rodríguez, amepokea tuzo hiyo ambayo imetolewa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas sambamba na tuzo nyingine ya bao bora la fainali za kombe la dunia mwaka 2014, ambalo alilifungwa wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Colombia dhidi ya Uruguay.
Tuzo ya goli bora la fainali za kombe la dunia za mwaka huu aliyokabidhiwa James David Rodríguez Rubio, ni viatu vya Adidas vyenye mfano wa toleo la sasa ambavyo vimetengenezwa kwa madini ya dhahabu.






FIFA wamemkabidhi tuzo hiyo Rudriguez mwenye umri wa miaka 23, ambayo ni kiatu cha dhahabu mjini Madrid ikiwa ni sehemu ya kutimiza makabidhiano ya zawadi kwa washindi mbali mbali wa fainali wa kombe la dunia za mwaka 2014.
Rodríguez, amepokea tuzo hiyo ambayo imetolewa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas sambamba na tuzo nyingine ya bao bora la fainali za kombe la dunia mwaka 2014, ambalo alilifungwa wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Colombia dhidi ya Uruguay.
Tuzo ya goli bora la fainali za kombe la dunia za mwaka huu aliyokabidhiwa James David Rodríguez Rubio, ni viatu vya Adidas vyenye mfano wa toleo la sasa ambavyo vimetengenezwa kwa madini ya dhahabu.






Thursday, August 14, 2014
Leo ni siku ya wanaotumia mkono wa kushoto duniani, fahamu maajabu ya watu hao kama Obama na Bill Gates.
Leo ni siku ya kimataifa ya watu wanaotumia mkono wa kushoto duniani kote ambayo miaka yote huadhimishwa August 13.
Siku hii maalum ilianzishwa kwa lengo la kutambua mchango na changamoto wanazokumbana nazo watu wanaotumia mkono wa kushoto dhidi ya wale wanaotumia mkono wa kulia.
Zipo facts zilizotolewa Marekani na wanasayansi kuhusu watu wanaotumia mkono wa kushoto nchini humo ambazo zinaweza kusaidia kutumika kama kielelezo kwa watu wengine.
Kwa mujibu wa ripoti ya wanasayansi wa Marekani, 10% ya raia wa nchi hiyo wanatumia mkono wa kushoto.
Utafiti unaonesha kuwa idadi kubwa zaidi ya watu wenye akili yenye uwezo wa ziada ‘Genius’ wanatumia mkono wa kushoto.
Marais watatu kati ya marais watano wa hivi kariibuni wa Marekani, wanatumia mkono wa kushoto. Yaani Barack Obama, Bill Clinton na Bush Sr.
Watu maarufu waliofanikiwa sana Marekani kama Albert Einstein, Bill Clinton, Oprah Winfrey, Leonardo da Vinci, Barack Obama na Bill Gates wanatumia mkono wa kushoto.
Kama wewe unatumia mkono wa kushoto, nakutakia siku njema na hongera.
‘Happy Left-Handers Day’
Monday, June 30, 2014
Hip Hop Ya Tanzania: Ni ubunifu au kubuni tu.
Chimbuko la Hip hop linaweza kufafanuliwa kwa kifupi kama ‘juhudi za wasiojiweza’. Hili lilionekana dhahiri wakati Wamarekani weusi walipokuwa wakipigania haki zao za kijamii, wakati huo wa civil rights movement. Hapa kwa haraka tunaona uhusiano wa Hip Hop na jamii. Hip Hop ikiwa upande wa wanyonge, ikitumika kama sauti ya wakandamizwaji.

Miaka hiyo imekwishapita na muziki huu umekua na kuwa ni utamaduni. Lakini bado umebaki na damu ya uanaharakati. Hip Hop imebadilika kama tamaduni yeyote ile, na mpaka kuvuka mipaka. Mipaka hiyo ilivuka hadi kufika Tanzania ambako ilikaribishwa. Boardman anajenga hoja kuwa, Hip Hop ilifanikiwa kuvuka mipaka ya Tanzania kutokana na kuanguka kwa Siasa ya Ujamaa. Mwanzo ulikuwa mgumu, na bado safari ni ndefu, lakini mafanikio yanaonekana; kama kukubalika na jamii.
Muziki huu hata hivyo bado unaonekana kama ni tamaduni ya Kimarekani zaidi, huku kuna baadhi ya watu kwenye jamii zetu ambao wanaona Hip Hop ya nyumbani ‘ina-recycle’ tu yale yanayofanywa na wasanii wa Marekani. Kwenye hilo natumaini kuwa kila mtu atakuwa na mawazo yake, lakini ili kupata jibu lililo karibu na sahihi, ni vizuri kurudi kwenye chimbuko la tamaduni wa muziki huu wa Hip Hop.
Muziki huu ulikuwa unaitwa “muziki wa kufokafoka” kipindi hicho. Nadhani hilo jina halikuwa sahihi, na uliupa mziki huu taswira mbaya. Lakini kwa kuwa ulikuwa ni muziki mpya, inawezekana hatukujua jina gani litakuwa sahihi. Hata hivyo, ukiangalia kwa karibu labda neno kufoka halikukosea sana, kwani kurap ni kama kufoka — lakini neno sahihi la Kiswahili ni kughani.
Muziki huu ulileta mgongano kati ya kizazi chetu na kizazi cha Tabora Jazz kwani muziki huu uliangaliwa kwa tafsiri tofauti. Muziki huu ulionekana ukiwa na hiyo dhana ya kufokafoka, na kawaida ya tamaduni zetu, mtoto hamfokei mzazi. Hivyo inawezekana Hip Hop ikaonekana ni muziki unaochochea uasi dhihi ya tamaduni zetu za ndio mzee. Lakini kwa upande mwingine, hasa ukiangalia katika chimbuko, huu ni muziki wa watu wanaokandamizwa. Hivyo kipindi kile cha akina II Proud na Wapi Tunakwenda, vijana tulikuwa na madukuduku mengi.

Hip Hop ikafanya vile vile kama ilichofanya Marekani kipindi cha miaka ya sitini na sabini — kuwapa wanyonge sauti. Tofauti ilikuwa, huko Marekani iliwapa watu weusi (hasa vijana) sauti dhidi ya ubaguzi wa rangi. Hapa Tanzania, suala halikuwa ubaguzi wa rangi, lakini kupigania haki za vijana, dhidi ya uonevu wa polisi, dhidi ya maisha magumu kwa vijana n.k. Hivyo ni kweli, mwanzoni kwenye hip hop watu walikuwa wanafoka vilivyo, kwani matatizo yalikuwa mengi na hakuna aliyewasilisha matatizo hayo ya vijana, au hata kuyapa nafasi ya kusikilizwa. Hilo linafanana na makundi kamaN.W.A. huko Marekani. N.W.A walikuwa wakali, kwani hali halisi yao ilikuwa ni ngumu sana kipindi hicho, ukilinganisha na sasa.
Sasa kama tamaduni nyingine, Hip Hop imekuwa inakwenda na wakati, pamoja na kuwa kwenda na wakati huko hakujasaidia sanaa hii moja kwa moja. Maisha yamebadilika, vijana wa juzi waliokuwa wanapigania haki zao, leo baadhi wamefanikiwa. Hivyo maudhui ya mashairi yamebadilika kwa namna moja au nyingine. Kama marekani, vijana wengi wametajirika kupitia mgongoc wa Hip Hop, hivyo kuanza kughani kuhusu utajiri wao, kwasababu hawaishi tena kwenyeghettos kama awali.
Hapa Tanzania, kwenye nchi masikini, Hip Hop imekuwa bado ikitegemewa katika kutetea haki za wanyonge na kuzungumzia matatizo ambayo yanaendelea kukabili vijana wengi. Pamoja wapo wachache, waliofanikiwa, wengi wa vijana bado wapo kwenye hali ngumu. Hapa ndipo neno “Hali Halisi” linapoingia katika kuchambua Hip Hop ya Tanzania. Wapo ambao wanahesabiwa kama si wana Hip Hop, kwani mashairi yao hayazungumzii hali halisi ya maisha ya kijana wa kila siku wa Kitanzania. Hili linaendana na picha zilizomo kwenye video nyimbo zao. Video nyingi zinaonekana kushindwa kuakisi yaliyomo katika tamaduni zetu, bali huakisi zaidi yaliyomo katika mila na desturi za tamaduni za Magharibi.
Hili suala la mila na desturi ni mjadala mwingine, kwani video hizi huonekana kama zinakiuka maadili ya mila na desturi zetu. Mengi yamezungumzwa, bila kufafanua nini maana ya mila na desturi zetu, kwani kama suala ni mavazi ya uchi,basi kuna Wamasai ambao hutembea wamevaa lubega tu, bila kuwa na mavazi ya ndani. Wapo wengine ambao wanaona picha za kwenye video za Hip Hop zinahamasisha maovu; kwa mfano ngono, kama vile video nyingi za Hip Hop za Marekani. Kama hilo ni tatizo, basi tunaweza kubadilishakituo cha runinga na kuweka mduara, ambao naamini ni tamaduni yetu.
Robben amekiri kujiangusha

Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti
Mshambulizi wa Uholanzi Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti ya ushindi lakini akasema alikuwa ametegwa .
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemkashifu refarii wa mechi yao na Uholanzi Pedro Proenca kwa kuipendelea Uholanzi .
Robben alikunguwa katika eneo la lango Uholanzi ilipokuwa imesawazisha bao moja kwa moja na ikaisaidia Uholanzi kuibuka mshindi kwa mabao 2-1 .Herrera amesema kuwa Penalti hiyo dakika tatu kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo haikufaa''hiyo ni njama ya FIFA kuiondoa Mexico kwenye kinyang'anyiro hicho .
Penalti hiyo ilifungwa na Jan-Klaas Huntelaar

Arjen Robben amekiri kuwa alidanganya timu yake ikapewa penalti
“nataka kwanza kuwaomba radhi mashabiki wangu kwa kudanganya na kujiangusha ukweli haikufaa '' Robben aliiambia runinga ya Uholanzi NOS.
''nafikiri kuwa refarii Proenca alifanya kweli kuashiria penalti akisema kuwa alikuwa ametegwa na nahodha wa Mexico Rafael Marquez.
Mexico ilikuwa imeongoza hadi dakika ya 88 ya kipindi cha pili kabla Wesley Sneijder kuisawazishia Uholanzi kabla ya Huntelaar kufunga penalti iliyozua ubishi mkubwa.
Herrera alisema kuwa haikufaa refarii kutoka ulaya alipewa mechi kati ya timu kutoka ulaya na Marekani ya kusini.
Kwanini FIFA hawakutupa refarii mwafrika mhindi ama hata refarii kutoka Marekani kusini ?
Friday, June 27, 2014
Thursday, June 26, 2014
Obama aomba pesa awasaidie waasi.

Rais wa Marekani, Barrack Obama ameliomba Bunge la Congress kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kugharamia mafunzo na kuwapatia silaha Waasi wa Syria.
Bado haijajuliakana ni aina gani ya msaada wa kijeshi ambao Marekani itautoa japo kulikuwa na maombi ya waasi hao wa Syria kuhusu kupewa makombora ya kubeba ya kutungulia ndege ambayo yalitupiliwa mbali kwa kuhofia silaha hizo zisiwaendee wanamgambo wa makundi ya kigaidi.
Ikiwa Bunge hilo litaridhia Ombi la Rais Obama,hii itakuwa mara ya kwanza kwa Jeshi la Marekani kujihusisha moja kwa moja kwenye mgogoro wa Syria, mashirika ya kiintelijensia ya Marekani tayari yanawasaidia waasi nchini Syria.
Waasi wa Syria wanapambana na wanajeshi wa serikali na wanamgambo wa ISIS, ambalo ni kundi la waislamu ambao pia wameteka mpaka ndani ya nchi ya Iraq.
Monday, June 23, 2014
Monday, June 16, 2014
Mwanamziki apasuliwa huku akiimba.

Alama Kante afanyiwa upasuaji
Katika tukio la kwanza la aina yake mwanamziki mmoja nchini Ufarasa amefanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe kooni huku akiimba.
Madaktari wanasema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuepuka kuharibu mishipa inayosaidia binadamu kutoa sauti.Mwimbaji huyo Alama Kante, ambaye ni raia wa Guinea anayeishi Ufaransa alipewa dawa za kumfanya asihisi uchungu wakati upasuaji huo ukiendelea.
Kante alikua na hofu kuhusu kupoteza sauti yake kutokana na upasuaji huo lakini daktari wake akapendekeza aimbe huku akipasuliwa ikiwa ni mara ya kwanza hatua kama hiyo kuwahi kuchukuliwa kote duniani.
Profesa Giles Dhonneur, aliyeongoza upasuaji huo katika hospitali ya Henri Mondor hospital, ameonyesha video ya mwanamziki huyo akiimba huku naye akiendelea na upasuaji. Ameelezea matuamani kuwa mambo yatakuwa sawa.
Amesema ni uchungu sana kufanya upasuaji kama huo bila kutumia dawa ya kumfanya mgonjwa asihisi uchungu lakini mbinu na dawa aliyotumia ilimuwezesha Kante kuhimili bila matatizo yoyote.
Kante ambaye amepata nafuu amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi kama yuko Senegal na alipoamka na kuzungumza tena madkatari na wauguzi walifurahi sana kutimiza lengo lao.
Ufaransa yafaidi teknolojia ya goal.

Ufaransa yafaidi Teknolojia ya kuwasaidia marefarii Brazil 2014
Ufaransa ndiyo timu ya kwanza
kuwahi kufaidi matumizi ya teknolojia ya kisasa kuzuia ubishi katika
mechi ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.
Karim Benzema alikuwa anatekeleza mashambulizi
katika lango la Honduras kunaklo dakika ya 48 ya kipindi cha pili lakini
kipa wa Honduras Noel Valladares akababaika na mpira ukavuka laini
kisha akaunyofoa mara moja naMashabiki na wachezaji wa Honduras waliokuwa ndani ya uwanja wa Porto Alegre walijaribu kupinga kauli ya refarii huyo lakini wapi alihakiki bao hilo la pili usiku huu kwa Ufaransa .
Honduras ilikuwa tayari imempoteza mchezaji wao Palacios mwisho wa kipindi cha kwanza alipoonyeshwa kadi ya pili ya manjano
Teknolojia hiyo inayotumika kwa mara ya kwanza inajumuisha kamera 14 za kisasa na zenye uwezo mkubwa wa kurekodi picha na sauti kwa kasi mno na mpira ambao inasambaza

Ufaransa yafaidi Teknolojia ya goaline dhidi ya Honduras Brazil 2014
Kamera hizi zimeunganishwa kwenye tarakilishi inayounda maumbo na kuondoa umbo lolote lile ambalo sio la mpira, kisha kufuata mwenendo wa mpira kwa kadri milimita chache, kampuni hiyo ilisema.
Mpira unapovuka tu mstari wa lango, utakuwa unapeperusha ujumbe kwenye saa yake mwamuzi wa mechi, kisha ujumbe wenye maandishi ‘GOAL’ unatokea kwenye saa hiyo pamoja na mtikisiko (Vibration).
Haya yote yanafanyika kwa muda wa chini ya sekunde moja.

Ufaransa yafaidi Teknolojia ya goaline dhidi ya Honduras Brazil 2014
Kampuni ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa, ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya michezo.
Hii itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa katika mfumo wa kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High Definition (UHD), ujulikanao kama 4K Format, ambayo kiwango chake ni mara nne zaidi ya kiwango cha
televisheni za kawaida.

Teknolojia yamsaidia refarii kuipa Ufaransa bao
Ni mfano mmoja tu wa jinsi kombe hili la dunia litakavyokua lenye teknolojia kubwa zaidi na lenye kujumuisha miundo mbinu ya teknolojia ya karne ya 21.
Tuesday, May 20, 2014
Rais Morales kucheza kiungo cha kati.

Rais Morales ni shabiki sugu wa kandanda
Hebu tafakari rais wa nchi kuchezea klabu ya kandanda inayoshiriki ligi ya taifa ya daraja la kwanza ?
Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili
rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo cha kati kuanzia Agosti
mwaka huu.Rais Morales atalipwa mshahara wa dola $213 kwa mwezi .
Morales atavalia jezi nambari 10 katika klabu hiyo iliyoko Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.
Mashabiki wanamsubiri kwa udi na uvumba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni shabiki sugu wa kandanda kushuka dimbani.
Rais huyo ambaye ni shabiki sugu wa kandanda na mwenye umri wa miaka 54 ataichezea Sports Boys, timu ilyoko kusini mashariki mwa mkoa wa Santa Cruz.
Timu hiyo iliyoko katika ligi ndogo ilisema kuwa rais huyo atakuwa akicheza angaa kwa dakika 20 katika kila mchuano, hasa ikizingatiwa kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi.
Rais wa klabu hiyo alisema kwamba rais huyo anapenda kandanda, na kwamba yeye hucheza vizuri.

Rais Evo Morales akiwa uwanjani
Edwin Tupa, mwanasiasa kutoka katika chama cha MAS, ambacho ndicho chama tawala nchini humo, alisema kuwa ndoto ya rais huyo ya kuchezea klabu ya kiitaaluma ilikuwa imetimia.
Inasemekana kuwa rais huyo yuko sawa na ni mwenye furaha katika matarajio yake ya kucheza kandanda.
Bwana Morales amewahi kucheza katika mechi nyingi iliyotambulika pamoja na wanahabari, viongozi wa umoja na marais wengine.
Mwaka wa 2007, rais huyo alishiriki katika mechi iliyokusudiwa kupinga kikwazo kilichokuwa kimewekewa Bolivia, cha kutoshiriki katika mechi za kimataifa katika sehemu zenye urefu.
Sunday, May 18, 2014
Arsenal mabingwa wa FA 2014.

Wachezaji wa Arsenal wakishangilia ushindi
Timu ya Arsenal ya England
imetwaa kombe la FA baada ya kubamiza Hull City kwa jumla ya magoli 3 – 2
kwenye fainali iliyofanyika katika uwanja wa Wembley siku ya jumamosi.
Katika mechi hiyo ya fainali Hull City ndio
waliokuwa wa kwanza kuutikisa wavu wa Arsenal kwa magoli mawili ya
haraka haraka yaliyofungwa ndani ya dakika 10 kipindi kwanza.
Goli la kwanza lilifungwa na James Chester dakika ya 3 huku goli la pili la Hull likifungwa katika dakika ya 7 na Curtis Davies.
Hata hivyo magoli hayo hayakuweza kudumu kwani katika dakika ya 16 Santiago Cazorla aliifungia Arsenal goli na hivyo hadi mapunziko matokeo yakawa 1 – 2.
Katika kipindi cha pili Arsenal walikuja juu na kusawazisha goli hilo katika dakika ya 80 lililofungwa na Laurent Koscielny na kuwa 2 – 2 na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike dakika 90 za kawaida kwa sare ya 2 - 2 bila kumpata bingwa.
Baadae mwamuzi wa mpambano huo Lee Probert aliongeza dakika nyingine 30 ambazo zilifanya Arsenal wajiongezee goli la tatu na la ushindi katika dakika ya 108 lililofungwa na Aaron Ramsey.
Hadi mpira unamalizika Arsenal wakawa wameifunga Hull City kwa jumla ya magoli 3 -2
Gunners ilishinda taji lake la mwisho mwaka 2005 katika fainali za kombe la F.A ambapo iliwacharaza wapinzani wao wa jadi Manchester United katika mechi iliochezewa katika uwanja wa Cardiff,huku timu ya Hull City ikishiriki kwa mara ya kwanza katika fainali ya kombe hilo.
Meneja Arsene Wenger ameshinda mataji saba muhimu katika miaka yake 18 kama mkufunzi wa timu ya Arsenal, ikiwemo mataji matatu ya ligi kuu ya uingereza pamoja na manne ya kombe la F.A.
Mashabiki wa timu zote mbili walikabidhiwa tiketi 25,000 kila mmoja huku tiketi nyengine 20,000 zikipewa watu waliojitolea katika mashirika ya hisani,vilabu na ligi za kaunti.
Hata hivyo magoli hayo hayakuweza kudumu kwani katika dakika ya 16 Santiago Cazorla aliifungia Arsenal goli na hivyo hadi mapunziko matokeo yakawa 1 – 2.
Katika kipindi cha pili Arsenal walikuja juu na kusawazisha goli hilo katika dakika ya 80 lililofungwa na Laurent Koscielny na kuwa 2 – 2 na hivyo kufanya mechi hiyo imalizike dakika 90 za kawaida kwa sare ya 2 - 2 bila kumpata bingwa.
Baadae mwamuzi wa mpambano huo Lee Probert aliongeza dakika nyingine 30 ambazo zilifanya Arsenal wajiongezee goli la tatu na la ushindi katika dakika ya 108 lililofungwa na Aaron Ramsey.

Gunners ilishinda taji lake la mwisho mwaka 2005 katika fainali za kombe la F.A ambapo iliwacharaza wapinzani wao wa jadi Manchester United katika mechi iliochezewa katika uwanja wa Cardiff,huku timu ya Hull City ikishiriki kwa mara ya kwanza katika fainali ya kombe hilo.
Meneja Arsene Wenger ameshinda mataji saba muhimu katika miaka yake 18 kama mkufunzi wa timu ya Arsenal, ikiwemo mataji matatu ya ligi kuu ya uingereza pamoja na manne ya kombe la F.A.
Mashabiki wa timu zote mbili walikabidhiwa tiketi 25,000 kila mmoja huku tiketi nyengine 20,000 zikipewa watu waliojitolea katika mashirika ya hisani,vilabu na ligi za kaunti.
5 wauawa katika mlipuko Nigeria.

Mlipuko wa bomu Nigeria
Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo
linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao
wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.
Mashambulio ya awali
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.
Monday, May 12, 2014
Boko H: Waonyesha wasichana waliotekwa.

Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram
Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa
nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya
Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo,
kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika
kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
Friday, May 9, 2014
Riadha ya Diamond League kuanza leo Doha.

Usain Bolt anayetarajiwa kushiriki riadha ya Diamond League itakayokuwa Doha, Qatar.
Ni Mashindano ya Riadha yanayopambwa na wakimbiaji nyota duniani na huu ni mkondo wa kwanza.
Kuna jumla ya mikondo 14 ya mbio hizi ambazo zitamalizika tarehe tano Septemba mwaka huu mjini Brussels, Ubelgiji.Mabingwa kama vile Usain Bolt , Yohan Blake huwa vivutio vikubwa lakini muhimu zaidi mashindano hayo ni jukwaa mojawapo kubwa la kuonyesha nyota wa Afrika mashariki na kati.
Miongoni mwa wanaotarajiwa kupeperusha bendera ya Afrika kama kawaida ni wa-Ethiopia kama vile Mohamed Aman na wakenya , akina Job Kinyor, Kipkorir Mutahi wanatarajiwa kumpa upinzani mkali Nijel Amos mshindi wa medali ya fedha mbio mita 800 katika olympiki iliyopita ya London kwani bingwa David Rudisha mkenya huenda asishiriki kwa sababu angali anauguza jeraha.
Katika mbio kama zile za mita 3000 kuruka viunzi, wake kwa waume wakenya hufanya vizuri lakini ushindani ni mkubwa.
Thursday, May 8, 2014
USAIN BOLT ASAKA VIATU VYAKE.

Viatu vya Bolt vinagharimu pauni elfu 20 hizo ni dola elfu 34 za kimarekani
Mwanariadha Usain Bolt hana raha, anatafuta viatu vyake vilivyoibwa.
Mwanariadha huyo bingwa wa Olympic wa mbio fupi
sasa ameeingia kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa twitter ulio na
zaidi ya mashabiki millioni 3 wanaomfuatilia, akisihi 'jamani najua si
tumarafiiki.., aliyeonea viatu vyangu au aliyenavyo tafadhali
uvirudishe'!Viatu hivyo vya michezo rangi ya chungwa chapa cha Puma ,alivyowiweka saini yake vinagharimu pauni za Uingereza elfu ishirini.
Majajusi wa Scotland Yard wanasema viliibwa wiki iliyopia mtaa wa Craydon huko London maeneo ya viwandani vilipokuwa vimeekwa kama maonyesho.
Pia nao wanasihi atakaekuwa na fununu yoyote kuvihusu apige ripoti polisi.
Picha za viatu hivyo alivyovaa Usain alipotwaa ushindi zimezagaa mitandaoni, na sasa anaweka saini pair nyengine atakayoipelekea huko Uingereza.
Wadadisi wanasema itabidi ulinzi wa viatu hivyo uimarishwe zaidi.
Wednesday, May 7, 2014
Mvua ya Samaki Sri Lanka.

Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali
Wakaazi wa kijiji kimoja
Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa
na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo.
Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.Wanakijiji hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu kizito kikianguka na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa
Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.

Wakazi wanasema sio mara ya kwanza kwa mvua ya Samaki kuwanyeshea
Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.
Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo badaye.
Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.
Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi wa Marekani na Uingereza.
Samaki wamadhamana kuu Sri Lanka.
Tuesday, May 6, 2014
MASHAIRI YA SHABIKI BY MANSU LI.
MANSU LI. |
what is it now
what is it now
Ubeti1:
Nilimuona shabiki tu ambaye ananikubali
na wala sikutaraji angeweza kufika mbali
mara miezi inapita tunajuana kiundani
Shabiki akawa rafiki anakuja mpaka nyumbani
Siri moyoni sielewi ana nia gani
mara akinikosa hewani kwake tafrani
kumbe shabiki alisha-fall in love
lakini ni too late men, oh my God
Anasema hawezi bila mimi
nilishamteka akili na hajui afanye nini
huku nae mamaa anahisi namzunguka
sio mimi wa zamani anadai na-change hulka
Shabiki gani anayepiga hata usiku
ukiuliza kwanini anasema i miss u
kwanini mamaa asipoteze amani
na huku anajua fika hili penzi limashakani
(kiitikio)
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
Ubeti2:
Anadai mara ya kwanza aliniona kwenye tv
kwenye video ya KINA KIREFU long T
kisha akaniona kwenye TUKO PAMOJA
na hapo ndipo akachoka kungoja
Siku ya siku ilikuwa kwenye show
akajikaza kisabuni pasina kuona soo
excuse me,inakuaje bro?
sio siri nimependa vile unavyo-flow
Nikasema asante kisha tukaachana
kumbe haikuwa mwisho baada ya kuagana
sijui ni wapi alipopata yangu namba
ndivyo hivyo akaanza kuniganda
Anataka tuchat saa zote
anasema ni mimi naemuondoa upweke
hata kama ninae anasema, i don't care
mazoea yana tabu na yeye alishanizoea
(kiitikio)
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
ubeti3:
You’re so cute
But I can’t be with you
sitaki kukuchezea halafu nikipe kitu
Maybe just a friendship kama kwako sio ishu
Please understand me I’ll never be with you
Sikujua ukweli unaosema ungezusha vita
Sms za matusi zikaanza miminika
Akunielewa alihisi tu naringa
Bora lawama acha anione mjinga
I keep gangster girl I keep it real
Am so sorry I can imagine how you feel
Vipi utajiskia nikiku nikakuacha
Am not a player am street hustler
Inataka moyo kuwa kioo cha jamii
Sometimes tunateleza sisi sio manabii
Hapa ndipo wengeni uzalendo unapowashinda
Na isiwe tabu basi wanafanya kibingwa
(kiitikio)
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
what is it now shabiki
you wanna be my baby
i dont real get what you want
what is it now shabiki
you wanna be my lady
i can never do that
MASHAIRI YA KIPIMO CHA PENZI AZMA FT KITA!

INTRO
ah ah ah aha ha ah EI ZED EM EI(AZMA) ah ah aha yo yo
VERSE I (AZMA)
Kila men anakuaproach, anataka mikasi,hujui cha kufanya,
Bora umurike kaa unatochi, ujue kipimo ni hasi ,au kipimo ni chanya,
Kama kipimo ni sex,mbona mmefanya wee, na bado mchizi akakuacha,
Kama dereva wa teksi,mbona umesanya wee, waka peez wakakuacha.
Kama love ni glass,basi tugonge chears,
Kama love ni class,basi tufute tears,
Ulishawahi kuwa na mpenzi,akakuacha solemba,
Akakugeuza kama mshenzi,ukavikwa kiremba,
Ukajuiuliza whats wrong, au sijui kupenda?
Unapaswa kuwa strong,japo walishakutenda,
Hakuna love chini ya jua,usiingie kichwa kichwa,
Ni bora leo uka jua,usiishie fichwa fichwa.
Mapenzi yamegeuka fimbo,wengi hatujui kutenda,
Uongofu umegeuka wimbo,wengi hatujui kupenda,
Anayekupenda kisa mwanya,uking’oa itakuwaje?
Anayekupenda unavyofanya ukimuoa itakuwaje?.
yeh u better think twice ah ha ha MUJWAHUKI.
Kila men anakuaproach, anataka mikasi,hujui cha kufanya,
Bora umurike kaa unatochi, ujue kipimo ni hasi ,au kipimo ni chanya,
Kama kipimo ni sex,mbona mmefanya wee, na bado mchizi akakuacha,
Kama dereva wa teksi,mbona umesanya wee, waka peez wakakuacha.
Kama love ni glass,basi tugonge chears,
Kama love ni class,basi tufute tears,
Ulishawahi kuwa na mpenzi,akakuacha solemba,
Akakugeuza kama mshenzi,ukavikwa kiremba,
Ukajuiuliza whats wrong, au sijui kupenda?
Unapaswa kuwa strong,japo walishakutenda,
Hakuna love chini ya jua,usiingie kichwa kichwa,
Ni bora leo uka jua,usiishie fichwa fichwa.
Mapenzi yamegeuka fimbo,wengi hatujui kutenda,
Uongofu umegeuka wimbo,wengi hatujui kupenda,
Anayekupenda kisa mwanya,uking’oa itakuwaje?
Anayekupenda unavyofanya ukimuoa itakuwaje?.
yeh u better think twice ah ha ha MUJWAHUKI.
CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
VERSE II AZMA
Je kipimo ni mita,au ni sentimita?
Je kipimo ni lita,au ni senti lita?
Aliyekupenda kwenye shida,itakuwaje kwenye rahaa?
Pasipo love ni kawaida,kuna kuachwa kwa mataa,
Walioana mchana,usiku wakatengana,
Walipendana kwa sana,hawakuweza kulindana,
Kama kipimo ni imani,wengi walishaaminiana na mwisho wakafumaniana,
Kama kipimo ni amani,wengi walisha ridhiana na mwisho wakatalikiana.
mpenzi anapozembea, ndio mwingine anapokata hamu,
Aanapenda unavyotembea, au anapenda unavyotabasamu,
Mnagombana kisa shory,anayemegwa kila dakika,
Mapenzi yamegeuka story,na hadithi za kusadikika,
Mliokutana kwenye baa,mnaoana kwenye gesti,
Mnainuka na kukaa,mlioshindwa kwenye testi,
Aliyeachana na mkewe,amemuoa house girl,
Usiombe ukawa ni wewe,unayegeuzwa tom and jelly,
Anayekupenda unamkataa, we unapenda kwingine,
Unayemuwaza kila saa, ye anamuwaza mwingine.
CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
VERSE II AZMA
Je kipimo ni mita,au ni sentimita?
Je kipimo ni lita,au ni senti lita?
Aliyekupenda kwenye shida,itakuwaje kwenye rahaa?
Pasipo love ni kawaida,kuna kuachwa kwa mataa,
Walioana mchana,usiku wakatengana,
Walipendana kwa sana,hawakuweza kulindana,
Kama kipimo ni imani,wengi walishaaminiana na mwisho wakafumaniana,
Kama kipimo ni amani,wengi walisha ridhiana na mwisho wakatalikiana.
mpenzi anapozembea, ndio mwingine anapokata hamu,
Aanapenda unavyotembea, au anapenda unavyotabasamu,
Mnagombana kisa shory,anayemegwa kila dakika,
Mapenzi yamegeuka story,na hadithi za kusadikika,
Mliokutana kwenye baa,mnaoana kwenye gesti,
Mnainuka na kukaa,mlioshindwa kwenye testi,
Aliyeachana na mkewe,amemuoa house girl,
Usiombe ukawa ni wewe,unayegeuzwa tom and jelly,
Anayekupenda unamkataa, we unapenda kwingine,
Unayemuwaza kila saa, ye anamuwaza mwingine.
CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
VERSE III (AZMA)
Wanakupenda kisura,ama kisa mavazi,
Mapenzi sio chakula,usifiche maradhi,
Mwanzo washakutapeli,ukabaki umesizi,
Wanakupenda kiukweli,hiyo bado ndio quiz,
Inakuwaje kama una mpenzi,mmeshamaliza sex,anataka umlipe,
Utajuaje kama kuna penzi,huduma imegeuka tex,upande na ulipe,
Kama kipimo ni mtoto,mbona umeshazalishwa na jamaa akasepa?
Kujua kipimo ni ndoto,uongo umeshahalalishwa wanakomaa na paper. love in epa, they love ur paper,
utapay price ukidata na foreign love,think twice before hujafall in love
kama kipimo ni tabia,mbona binti malkia,kaolewa n a muuza gongo?
Waliokutana kwenye bia,leo washanitamkia,penzi lao sio la uongo.
Kuna ulimbo,kwani urembo,umegeuzwa biashara,
Kutoka chimbo,we ni gembo,unanasa kwa ishala,
Wangapi ushawadanganya,eti usiku haujalala?
Wangapi ushawachanganya,haya mapenzi ni jalala?
CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
VERSE III (AZMA)
Wanakupenda kisura,ama kisa mavazi,
Mapenzi sio chakula,usifiche maradhi,
Mwanzo washakutapeli,ukabaki umesizi,
Wanakupenda kiukweli,hiyo bado ndio quiz,
Inakuwaje kama una mpenzi,mmeshamaliza sex,anataka umlipe,
Utajuaje kama kuna penzi,huduma imegeuka tex,upande na ulipe,
Kama kipimo ni mtoto,mbona umeshazalishwa na jamaa akasepa?
Kujua kipimo ni ndoto,uongo umeshahalalishwa wanakomaa na paper. love in epa, they love ur paper,
utapay price ukidata na foreign love,think twice before hujafall in love
kama kipimo ni tabia,mbona binti malkia,kaolewa n a muuza gongo?
Waliokutana kwenye bia,leo washanitamkia,penzi lao sio la uongo.
Kuna ulimbo,kwani urembo,umegeuzwa biashara,
Kutoka chimbo,we ni gembo,unanasa kwa ishala,
Wangapi ushawadanganya,eti usiku haujalala?
Wangapi ushawachanganya,haya mapenzi ni jalala?
CHORUS (KITA)
Tell me,(tell me) kipi kipimo cha penzi,i wanna know just tell me.(tell me)
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
kipi kipimo cha penzi, mi nijue
Tahadhari kwa wezi wa simu mitaani!

Mwizi aliyepigwa picha na simu hiyo ya HTC
Simu ya mkononi iliyokuwa imeibwa, ilituma ujumbe mfupi na picha ya mwizi wa simu hiyo kuonyesha kuwa ndiye mmiliki wake.
Polisi katika eneo la Essex nchini Uingereza wanamtafuta mwizi wa simu hiyo.Simu hiyo aina ya HTC, iliibwa kutoka kwa koti la mwanafunzi mmoja alipokuwa safarini kuelekea nyumbani.
Mwenye simu alikuwa ameweka kifaa cha usalama kwenye simu hiyo ambacho kinaifanya simu kumpiga picha mtu anapojaribu kuingiza nambari ya siri au PIN mara tatu bila kufanikiwa.
Msemaji wa polisi alisema kuwa simu hiyo ilimpiga picha mwanamume huyo alipojaribu kuingiza nambari hiyo bila kufanikiwa.
Barua pepe ya mwanafunzi huyo ilituma ujumbe kwa polisi kuwaarifu kuhusu wizi huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)