Kwa mujibu Fareed Kubanda aka Fid Q, ‘Bongo Hiphop’ ni msichana
anayempenda kwa dhati na wataishi pamoja katika shida na raha. Fid
ameonesha msimamo huo kwenye wimbo wake mpya ‘Bongo Hiphop’ aliouchia
kwenye siku yake ya kuzaliwa (August 13) na kumshirikisha producer
mkongwe, P-Funk Majani.
Kwenye wimbo huo, Ngosha anaelezea jinsi ambavyo hiphop ya Tanzania
ilianza kabla ya Bongo Flava japo wasanii wa hiphop wengi hawafaidiki
kiuchumi ukilinganisha na wasanii wanaoimba.
“Bongo Flava mzuri kiasi hiphop wewe ndio my queen, my first, my
last and everything in between,” anarap Fid. “Kama kukupenda wewe ni
dhambi basi shetani yu nami, na kamwe sitonyea kambini ili niwabambe
dukani,” anasikika rapper huyo.
Pamoja na wimbo huo, Fid pia ataachia documentary yenye jina hilo
(Bongo Hiphop) ambayo itazungumzia historia ya muziki wa hiphop nchini.
No comments:
Post a Comment