facebook

Thursday, August 21, 2014

Fid Q aifafanisha ‘Bongo Hiphop’ na msichana anayempenda kwa dhati kwenye wimbo mpya.

Kwa mujibu Fareed Kubanda aka Fid Q, ‘Bongo Hiphop’ ni msichana anayempenda kwa dhati na wataishi pamoja katika shida na raha. Fid ameonesha msimamo huo kwenye wimbo wake mpya ‘Bongo Hiphop’ aliouchia kwenye siku yake ya kuzaliwa (August 13) na kumshirikisha producer mkongwe, P-Funk Majani.
Kwenye wimbo huo, Ngosha anaelezea jinsi ambavyo hiphop ya Tanzania ilianza kabla ya Bongo Flava japo wasanii wa hiphop wengi hawafaidiki kiuchumi ukilinganisha na wasanii wanaoimba.
“Bongo Flava mzuri kiasi hiphop wewe ndio my queen, my first, my last and everything in between,” anarap Fid. “Kama kukupenda wewe ni dhambi basi shetani yu nami, na kamwe sitonyea kambini ili niwabambe dukani,” anasikika rapper huyo.
Pamoja na wimbo huo, Fid pia ataachia documentary yenye jina hilo (Bongo Hiphop) ambayo itazungumzia historia ya muziki wa hiphop nchini.

Mfahamu Jyoti, mwanamke mfupi zaidi duniani 'Sentimita 60' anaepata deals kubwa Marekani.

Rais wa Colombia aunga mkono Bhangi.

Rais wa Colombia aunga mkono kuhalalishwa kwa Bhangi
Rais wa Colombian Juan Manuel Santos amesema kuwa anaunga mkono matumizi ya bangi kwa minajili ya utabibu.
Bwana Santos ameunga mkono mswada ambao utapigiwa kura bungeni wakati wowote kwa manufaa ya kupunguza uchungu kwa wagonjwa .
Rais wa Colombia aunga mkono kuhalalishwa kwa Bhangi
Rais huyo amesema kuwa kuhalalishwa kwa Bangi kutawanyima walanguzi wa mihadarati biashara kwani itakuwa sio haramu kupatikana na bangi nchini humo.
Colombia ni moja kati ya mataifa ambayo yamekumbwa na vita vya walanguzi wa madawa ya kulevya na serikali vita ambavyo vimesababisha mauaji ya mamia ya watu. .
Marijuana inakuzwa kwa wingi nchini Colombia, lakini taifa hilo linajulikana kote duniani kwa ukuaji wa cocaine, kwa pamoja na Peru.
Bhangi inakuzwa kwa wingi nchini Colombia
Asilimia kubwa ya madawa hayo kulingana na takwimu yanauzwa nchini Marekani ambapo yanaingizwa kisirisiri kupitia mataifa ya Marekani ya kati na Mexico.
"natumai tutaliangazia jambo hili la matumizi ya marijuana kwa mtazamo mpya utakaofaidi wagonjwa ambao wanaitegemea kupunguza uchungu.'' alisema bwa Santos akiwa mjini Bogota.

Friday, August 15, 2014

Picha: Adidas na FIFA wamkabidhi James Rodriguez mzigo wa dhahabu.

Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limekabidhi tuzo ya mfungaji bora wa fainali za kombe la dunia zilizohitimishwa nchini Brazil July 13 mwaka huu, mshambuliaji kutoka nchini Colombia na klabu ya Real Madrid James David Rodríguez Rubio.
FIFA wamemkabidhi tuzo hiyo Rudriguez mwenye umri wa miaka 23, ambayo ni kiatu cha dhahabu mjini Madrid ikiwa ni sehemu ya kutimiza makabidhiano ya zawadi kwa washindi mbali mbali wa fainali wa kombe la dunia za mwaka 2014.
Rodríguez, amepokea tuzo hiyo ambayo imetolewa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas sambamba na tuzo nyingine ya bao bora la fainali za kombe la dunia mwaka 2014, ambalo alilifungwa wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Colombia dhidi ya Uruguay.
Tuzo ya goli bora la fainali za kombe la dunia za mwaka huu aliyokabidhiwa James David Rodríguez Rubio, ni viatu vya Adidas vyenye mfano wa toleo la sasa ambavyo vimetengenezwa kwa madini ya dhahabu.






Thursday, August 14, 2014

Leo ni siku ya wanaotumia mkono wa kushoto duniani, fahamu maajabu ya watu hao kama Obama na Bill Gates.

Leo ni siku ya kimataifa ya watu wanaotumia mkono wa kushoto duniani kote ambayo miaka yote huadhimishwa August 13.
Siku hii maalum ilianzishwa kwa lengo la kutambua mchango na changamoto wanazokumbana nazo watu wanaotumia mkono wa kushoto dhidi ya wale wanaotumia mkono wa kulia.
Zipo facts zilizotolewa Marekani na wanasayansi kuhusu watu wanaotumia mkono wa kushoto nchini humo ambazo zinaweza kusaidia kutumika kama kielelezo kwa watu wengine.
Kwa mujibu wa ripoti ya wanasayansi wa Marekani, 10% ya raia wa nchi hiyo wanatumia mkono wa kushoto.
Utafiti unaonesha kuwa idadi kubwa zaidi ya watu wenye akili yenye uwezo wa ziada ‘Genius’ wanatumia mkono wa kushoto.
Marais watatu kati ya marais watano  wa hivi kariibuni wa Marekani, wanatumia mkono wa kushoto. Yaani Barack Obama, Bill Clinton na Bush Sr.
Watu maarufu waliofanikiwa sana Marekani kama Albert Einstein, Bill Clinton, Oprah Winfrey, Leonardo da Vinci, Barack Obama na Bill Gates wanatumia mkono wa kushoto.
Kama wewe unatumia mkono wa kushoto, nakutakia siku njema na hongera.
‘Happy Left-Handers Day’