facebook

Wednesday, May 29, 2013

Onyo la tume kuhusu mishahara ya wabunge!

Maandamano ya kupinga wabunge kujiongeza mishahara mjini Nairobi
Tume ya mishahara nchini Kenya, imesema kuwa makarani wa bunge wenye jukumu la kuwalipa mishahara wabunge huenda wakapatikana na hatia ya kutumia vibaya mamlaka yao na kufuja pesa za umma ikiwa watawalipa mishahara ya juu wabunge kinyume na ile iliyoratibiwa na tume hiyo katika gazeti rasmi la serikali.


Mwenyekiti wa tume hiyo, Sarah Serem ameonya kuwa makarani wa bunge la taifa Justin Bundi na yule wa Senate, Jeremiah Nyegenye huenda wakapatikana na hatia ya matumizi mabaya ya mamlaka ikiwa watakiuka agizo hilo.
katiba inatupa mamlaka ya kuratibu mishahara ya maafisa wa serikali. Na hivyo ndivyo tulivyofanya,'' alisema mwenyekiti wa tume hiyo Bi Serem. Bi Serem alisema kuwa tume hiyo ilichapisha mishahara watakayopokea wabunge kwenye gazeti rasmi la serikali kwa nia nzuri.
"SRC haikushurutishwa kuchapisha taarifa hiyo katika gazeti rasmi la serikali. Lakini tuliamua kufanya hivyo kwa njia njema na ili wananchi waweze kupata habari hiyo.'' aliongeza Bi Serem
Tume hiyo hata hivyo iliwapongeza Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwa kusisitiza kuwa serikali ipunguze matumizi ya pesa za uma.
Bi Serem alisema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa na wawili hao ili kutenga pesa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Onyo la tume limekuja siku moja baada ya wabunge kupiga kura kupinga tangazo la tume hiyo kwenye gazeti rasmi la serikali kuhusu kiwango cha pesa watakachopokea wabunge.
Tangazo hilo lilisema kuwa kila mbunge atapokea shilingi laki tano za Kenya ambazo ni dola elfu sita. Wabunge hao wanapigania kulipwa dola elfu kumi na kuwafanya kuwa miongoni mwa wabunge wanaopokea kiasi kikubwa sana cha mishahara duniani

Mtoto alianguka kwa bahati mbaya China!

Mtoto mchanga aliyeokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka nchini China, alianguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya, mamake mtoto huyo amesema.


Mama huyo ambaye bado hajatajwa jila lake, aliambia polisi kuwa alijifungua mwanawe akiwa chooni na kuwa mtoto huyo aliteleza na kuanguka ndani ya bomba hilo kwa bahati mbaya
Mama huyo anaripotiwa kuangua kilio cha mwanawe , licha ya kuwa hakukubali kuwa ni mwanawe hadi baadaye.
Mtoto huyo anapokea matibabu hospitalini baada ya kuokolewa kutoka ndani ya bomba la maji taka. Bomba hilo lilikatwa kwa ustadi baada ya majirani kusikilia kilio cha mtoto huyo mjini Jinhua Jumamosi.
Shirika la habari la Zhezhong, lilisema kuwa mamake mtoto huyo mwenye umri wa miaka 22, aliambia polisi kuwa hangeweza kumudu gharama ya kuavya mimba. Hajaolewa na aliiweka mimba yake kuwa siri kubwa.
Alisema kuwa alijaribu kumzuia mtoto wake kuanguka baada ya kujifungua kwa ajali akiwa hospitalini lakini alianguka ndani ya bomba. Hata hivyo alimweleza mpangaji wake kulingana na shirika la habari la Xinhua.
Mama huyo alisema hakuwa na uwezo wa kumlea mwanawe kwa hivyo hakuambia yeyote kuwa ni mwanawe. Hata hivyo baadaye alijitambulisha na kuambia polisi ni mwanawe baada ya kuokolewa kwake.
Bomba aliloanguka ndani mtoto huyo
Polisi wanachunguza ikiwa tukio hilo lilikuwa la ajali au kilikuliwa kitendo cha maksudi.
Mtoto huyo alipatikana ndani ya bomba lenye urefu wa nchi nne
Alipata majeraha madogo kichwani na mikononi lakini anaendea kupata matibabu.
Kisa hicho kimezua mjadala mkali kwenye mitandao ya China huku baadhi wakisema kuwa mtoto huyo alikuwa ametupwa na mamake kwa maksudi.
Sheria za China za kupanga uzazi ni kali mno huku familia ikiruhisiwa kuzaa mtoto mmoja pekee na wazazi wanaweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini ikiwa watapatikana na hatia ya kupata zaidi ya mtoto mmoja.

Wafungwa kwa kushambulia ubalozi Tunisia!

Mahakama nchini Tunisia imewapa watu 20 kifungo cha nje cha miaka miwili kila mmoja kwa kuhusika na shambulizi dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Tunis, Septemba mwaka 2012, mawakili wa watu hao wamesema.


Watu wanne walifariki katika vurugu wakati ubalozi wa Marekani na shule moja jirani, ziliposhambuliwa.
Waandamanaji wa kiisilamu walilenga kushambulia ubalozi huo wakati yalipofanyika maandamano kupinga kutengezwa kwa filamu ya kiisilamu iliyomkejeli Mtume Mohammad nchini Marekani.
Katika miezi ya hivi karibuni serikali imekuwa na msimamo mkali dhidi ya watu wenye itikadi kali.
Mapema mwezi huu mtu mmoja aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji aliuawa wakati polisi walipokabiliana na wafuasi wa vuguvugu la Ansar al-Sharia mapema mwezi huu, viungani mwa mji mkuu Tunis.
Wakili wa washtakiwa, Anwar Oued Ali, aliambia shirika la habari la AFP, kuwa watashauriana na familia zao ikiwa wanataka kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.
Ikiwa wanataka tutafanya hivyo.
Hakuna tangazo rasmi kuhusu hukumu hiyo.
Pia jumanne mwanamume mmoja alifariki katika makabiliano kati ya polisi na wachuuzi, mjini Bizerte kuhusu sheria za uchuuzi.
Waziri wa mambo ya ndani alisema kuwa wachuuzi waliwarushia mawe polisi na mabomu ya petroli, ambapo polisi nao walijibu kwa kuwarushia gesi ya kutoa machozi.
Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mwanamume huyo alifariki kutokana na moshi.
Mapinduzi ya kiraia yaliyomng'oa mamlakani rais Zine El Abidine Ben Ali mwezi Januri, mwaka 2011 yalichochea wananchi wa nchi jirani kuandamana na kupinga serikali zao

Tuesday, May 28, 2013

Sudan yatisha kufungia Sudan.K mafuta!

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ametishia, kufunga kabisa bomba la mafuta ambalo husafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini hadi pwani ya Sudan, Red Sea.


Alisema kuwa Sudan itasitisha usafirishwaji wa mafuta ikiwa Sudan Kusini haitakoma kuwaunga mkono waasi wanaoendesha harakati zao katika eneo la mafuta la Sudan.




Jeshi la Sudan linapambana na waasi katika angalao maeneo matatu ya nchi hiyo.

Licha ya Sudan Kusini kujitawala mwaka 2011, hali ya wasiwasi kuhusu mafuta na ardhi imekuwa ikiendelea.
''Na sasa natoa onyo la mwisho kwa ndugu zetu wa Sudan Kusini kuwa tutafunga kabisa bomba la mafuta ikiwa wataendelea kuunga mkono wasaliti katika jimbo la Darfur , Kordofan ya Kusini na Blue Nile'' alisema Bashir kupitia televisheni ya taifa huku akigusia waasi wanaoendesha harakati zao katika maeneo hayo.
Kundi la waasi lenye mirengo mingi, linalojulikana kama Sudan Revolutionary Front (SRF), limefanya mashambulizi katika miji kadhaa huku wakiteka mji mkubwa wa Um Rawaba , katikati mwa Sudan mwezi Aprili.
Kundi hilo linalonuia kuipindua serikali ya rais Bashir, lakini wakaendelea kudhibiti mji wa Abu Kershola, katika eneo jirani la Kordofan Kusini.
Waasi wa SPLM-North walijiunga na kundi la waasi la JEM kutoka Darfur pamoja na makundi mengine ambayo ni ya mrengo wa (SLA), kwa lengo la kubuni kundi la
Sudan Revolutionary Front mwaka jana.
Rais Bashir alitoa hotuba yake moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa nchini Sudan, kufuatia tangazo la jeshi kuwa limeweza kuteka tena mji wa Abu Kershola kutoka kwa waasi.
Wakati huohuo, msemaji wa waasi hao aliambia shirika la habari la AFP kuwa wapiganaji waliondoka kutoka, eneo la Abu Kershola ili kulegeza vikwazo vya serikali kwa wenyeji wa eneo hilo.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukitetereka tangu mwaka 2011, wakati Sudan Kusini ilipoamua kujitawala.
Maswala muhimu kuhusu Uzalishaji wa mafuta, mizozo ya mipaka ynagali kutatuliwa.

TAARIFA KUHUSU MSIBA WA NGWAIR KUTOKA KWA BABA MDOGO WA MAREHMU!

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangwair ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani Baba Mkubwa wa Ngwair, David Mangwair ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach.Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini Baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na Kaka yake yaani Baba Mkubwa wa marehemu.Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Africa ya Kusini Baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili hup utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na Ubalozi wa Africa ya Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho Baba mdogo na Baba Mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.
;Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangwair ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani Baba Mkubwa wa Ngwair, David Mangwair ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach.Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini Baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na Kaka yake yaani Baba Mkubwa wa marehemu.Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Africa ya Kusini Baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili hup utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na Ubalozi wa Africa ya Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho Baba mdogo na Baba Mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.

Monday, May 27, 2013

Viongozi wa AU waanza mazungumzo!

Baada ya sherehe za Jumamosi mjini Addis Ababa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, viongozi wa Afrika sasa wanajadili baadhi ya matatizo yanayokabili bara hilo.


Vita vya muda mrefu katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo vilichukua nafasi kubwa mazungumzo yalipoanza.
Tena majadiliano yakahusu pendekezo la kuyafanya mahakama ya jinai ya kimataifa, ICC, yaache hatua za kumfikisha mahakamani rais mpya wa Kenya na makamo wake kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.
Wanabalozi wanasema viongozi wa Afrika wamegawika kuhusu swala hilo.
Mawaziri wa Mashauri ya Nchi za Nje walikubaliana Alkhamisi, kabla ya viongozi kukutana, kwamba AU iiombe ICC kupeleka jukumu la kesi za Rais Uhuru Kenyatta na makamo wake Wiliam Ruto kwa mahakama ya Kenya

ICC yatuhumiwa kwa ubaguzi wa rangi!


Uhuru Kenyatta alichaguliwa kama rais wa nne wa Kenya mwezi Mach

Muungano wa Afrika umeituhumu mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kuwaandama wafrika kwa sababu ya rangi yao.


AU inapinga hatua ya ICC kusisitiza kusikiliza kesi za washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu.




Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn aliyasema hayo akiongeza kuwa italalamika mbele ya Umoja wa Mataifa kuhusu hilo.

Rais Kenyatta anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Julai kusikiliza mashtaka dhidi yake kuhusu uhalifu dhidi ya binadamu.
Aidha Kenyatta amekanusha tuhuma hiuzo ambazo zinatokana na madai ya kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007 ambapo maelfu walipoteza maisha yao na wengine kuachwa bila makao.
Alichaguliwa kama Rais katika uchaguzi uliofanyika mwezi Machi na kumshinda mpinzani wake mkubwa Raila Odinga katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.
Akihutubia kikao cha marais wa Afrika kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa , bwana Hailemariam alisema kuwa viongozi wa Afrika wameelezea wasiwasi kuwa asilimia 99 ya wale wanaotakikana na mahakama ya ICC kwa makosa yoyote yale ni waafrika.
"hii ni dalili ya kuwa mambo sio sawa, mfumo wa ICC una hujuma,'' alisema bwana Hailemariam
Mahakama ya ICC ilibuniwa ili kuangamiza kile kilichoonekana kuwa viongozi wanaofanya uhalifu bila kujali, lakini sasa ''mfumo huo umegeuka na kuwa mfumo wa kuwaandamana watu kwa misingi ya rangi,'' alisema bwana Hailemariam.
''Mahakama ingali inawataka Kenyatta na Ruto licha ya jamii zao zilizokuwa na uhasama katika uchaguzi wa 2007 kuungana na kuwachagua wawili hao kuwa viongozi wa Kenya,'' aliongeza bwana Hailemariam.
Bwana Kenyatta na Bwana Ruto walikuwa wapinzani wakuu katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2007 ambo ulifuatwa na mauaji ya watu 1,000 na wengine laki sita kuachwa bila makao.
Wadadisi wanasema kuwa kesi za ICC ziliwapatanisha wawili hao kushikrikiana katika uchaguzi wa 2013, kwani waliamini kuwa jamii ya kimataifa ilikuwa inaingilia maswala ya ndani ya Kenya

Friday, May 24, 2013

Fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya!


Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borussia Dortmund
Fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani vitakavyokutana kwenye fainali.
Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko tayari pia.
Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.
Kocha wa Bayern Munich
Badala ya vilabu vya Uhispania na Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi kumiliki vilabu.

Soka imeimarika Ujerumani?

Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote, mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi, hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya kurekebisha hali hiyo.
Kocha wa Borussia Dortmund
Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.
Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya.

Tuesday, May 21, 2013

THE RETURN OF THE TRANS4M MASTER MIXX VOL 1. MUITE DVJ D OMMY. ..KUNA MIXING NA CUTING ZA AJABU ON TURNTABLEZ NI DVJ D OMMY,,,!

                                          http://www.hulkshare.com/­24piu8i0sirk

SOMA HISTORY YA MUZIKI WA HIP HOP!


Muziki wa hip hop ni aina ya muziki ulioanza kunako miaka ya 1970, ukiwa umeanzishwa na Wamarekani weusi katika miji mikubwa ya Marekani. Hip hop mara nyingi inatumia staili moja ya kuimba iitwayo kurap au kufokafoka.


Kurap ni staili ya uimbaji ambayo mwimbaji anatoa au anaimba maneno-mashairi yaambatanayo na vina. Mashairi mengi yaliyoimbwa katika muziki wa hip hop yalikuwa yakizungumzia maisha halisi ya watu weusi wa nchini Marekani, sanasana katika miji mikubwa.
Kuna baadhi ya mashairi ya muziki wa hip hop yanazungumzia wahuni, uharifu, na utumiaji haramu wa madawa ya kulevya. Muziki wa hip hop pia huchukua tabia (mwenendo) wa staili za muziki wa pop, yaani kama disko na reggae.  Itaendelea.........................!

Mwana Harakati PROFESA JAY AJIUNGA NA CHADEMA!

Profesa Jay
Mwana harakati PROFESA JAY ajiunga na CHADEMA.

Monday, May 20, 2013

Kagame akosoa kikosi cha UN DRC!

Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa mtazamo mkali wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kagame ameiambia BBC kwamba kikosi cha Umoja wa Mataifa cha askari elfu 20 kilichopelekwa miaka 14 iliyopita, hakijafanya lolote kutatua chanzo cha matatizo ya Congo na wakati mwingine kimeufanya mzozo huo kuwa mmbaya zaidi.
Amesema visa vya mapigano , ghasia, na watu kupoteza makaazi yao kulitishia usalama wa eneo zima.
Serikali ya rais Kagame imekana mara kwa mara tuhuma za Umoja wa mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba Rwanda inawasaidia wanamgambo mashariki mwa Congo.
Rais Kagame amesema kuwa kutumia nguvu kungesaidia ikiwa tu inekuwa inalenga kusaidia msimamo fulani wa kisiasa.

Wanne wafa kwenye msongamano kanisani!

Watu wane wamekufa na 13 kujeruhiwa katika mkanyagano ndani ya kanisa la kiavengalisti nchini Ghana.

Ajali hiyo ilitokea pale waumini walipoania kufikia maji matakatifu katika tawi la kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) katika mji mkuu, Accra.
Ripoti zinasema maelfu ya watu walikuwa wamekwenda kanisani humo.
Kanisa hilo liloanzishwa na kasisi wa Nigeria, TB Joshua, ambaye anasema yeye ni mtume.
Piya amezusha utata kwa kudai kuwa anaweza kutibu magonjwa yasiyotibika kama HIV na UKIMWI.

Wednesday, May 15, 2013

EU yachangisha kusaidia serikali ya Mali!

Zaidi ya wajumbe 100 wanakutana mjini Brussels, Ubeljiji kuchangisha fedha kutolewa kama msaada utakaotolewa kwa nchi ya Mali.     



Hili ndilo kongamano la kwanza tangu wanajeshi wa Ufaransa kuanzisha opesheni kazkazini mwa Mali dhidi ya wapiganaji wa kiiisilamu waliotwaa nusu ya maeneo ya nchi.

Wapiganaji hao walifanikiwa kuthibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali kutokana na udhaifu wa serikali iliyolaumiwa kuwa kujihusisha zaidi na ufisadi. Kipao Mbele kwa sasa ni jinsi ya kufanya mageuzi kwenye jeshi na tasisi nyingine za taifa.Wanajeshi wa Ufaransa waliingia ndani ya Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda.
Kumekua na shinikiza kwa Mali kuandaa uchaguzi mkuu wa kidemokrasia ifikapo mwezi Julai, japo raia wengi wameelezea ugumu wa kuafikiwa hilo.
Shirika la misaada la Oxfam limesema kwamba Mali itahitaji msaada kwa miaka 15 ijayo, ili kuafikia malengo yanayotarajiwa.
Licha ya juhudi za sasa, kungali na msukosuko wa kisiasa Mali, Kaskazini mwa Mali waafrika Weusi wamelalamikia kugabuliwa na jamii za kiarabu na Tuareg.
Kwa upande mwingine Tuareg na Waarabu wamelalamikia kubaguliwa na serikali Kuu iliyoko Bamako. Wafadhili wanasema ni muhimu kuwepo, na maridhiano kati ya jamii zote.mak

Waana Harakiti wa laani Kitendo cha kula Moyo Syria!

Hali imeendelea kuwa mbaya zaidi nchini Syria.
 Kanda ya video ambayo inaonekana kuonyesha muasi mmoja nchini Syria akila Moyo wa mwanajeshi aliyefariki, imelaaniwa vikali.      



Shirika la Marekani la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, limemtaja muasi huyo kama Abu Sakkar, muasi anayejulikana sana kutoka mji wa Homs, na kusema kuwa vitendo vyake ni vya uhalifu wa kivita.
Chama rasmi cha upinzani nchini Syria kimsema kuwa mshukiwa huyo lazima atakabiliwa na kesi mahakamani.
Kanda hiyo ambayo haiwezi kuthibitishwa , imeonyesha akikata moyo wa mwanajeshi huyo na kuula.
"naapa kwa Mungu, tutakula mioyo yenu na figo zenu , nyinyi wanajeshi wa Bashar,'' alisema muasi huyo akimtaja rais Bashar al-Assad wakati akiwa kando ya maiti ya mwanajeshi huyo.
Shirika la Human Rights Watch, linasema kuwa Abu Sakkar ni kiongozi wa kundi linalojulikana kama Omar al-Farouq Brigade.
"ukataji wa miili ya maadui ni uhalifu wa kivita, lakini la kuudhi zaidi ni swala la ghasia na vita kukithiri,'' alisema Peter Bouckaert wa shirika la HRW.
HRW limesema kuwa,wanaofanya uhalifu kutoka pande zote, lazima wajue kuwa watawajibishwa.
Aidha shirika hilo limesema kuwa Abu Sakkar aliwahi kunaswa kwa kanda ya video akirusha makombora katika maeneo yenye madhehebu ya Shia nchini Lebanon na kisha kusimama kando ya maiti ya wanajeshi waliouawa katika mashambulizi ya kuvizia.
Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao siku ya Jumapili, ni moja ya video inazoonyesha picha mbaya zaidi kuwahi kuonyeshwa tangu kuanza kwa vita vya Syria miaka miwili iliyopita.
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu 70,000, wameuawa tangu kuanza mapinduzi ya kiraia dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-Assad Machi 2011, ingawa baadhi ya mashirika yanasema idadi hiyo imefika watu 80,000.


Mwana Harakati Hayati Patrice Lumumba atunukiwa mji!

Lumumba alichaguliwa kama waziri mkuu wa DRC mwaka 1960
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatarejiwa kujenga mji ambao utakuwa kumbukumbu na kwa mpiganiaji uhuru wa nchi hiyo Patrice Lumumba . Hii ni kwa mujibu wa msemaji wa serikali Lambert Mende.      



Lumumba aliongeza kuwa, mji huo utakaojulikana  kama Lumumbaville utazileta pamoja jamii mbili zilizoko katika eneo hilo.
Lumumba aliyekuwa mshirika wa nchi za muungano wa Kisovieti, alichaguliwa kama waziri mkuu mwaka 1960, baada ya zaidi ya karne moja ya utawala wa kikoloni.
Mauaji yake, yalitokea miezi minne baadaye alipokuwa na umri wa miaka 35 na Marekani na Uingereza ndizo zililaumiwa kwa kifo chake.
Mwezi Aprili, mmoja wa wabunge wa bunge la malodi nchini Uingereza alisema kuwa afisaa mmoja wa MI6, alimwambia kuwa Uingereza ilihusika na kifo cha Lumumba.
Mwandishi wa BBC mjini Kishansa anasema kuwa habari hii bila shaka itapokelewa vyema na wananchi wa DRC kwani Lumumba anasalia kuwa mtu mashuhuri.
Mji wa Lumumbaville utajengwa katika mkoa wa Kassai-Oriental ambako alizaliwa hayati Lumumba.
Ujenzi wa mji huo unatarajiwa kuanza mwaka 2014, aliongeza kusema bwana Mende.
Serikali inatumai kuwa wahisani watasaidia katika ujenzi wa mji huo na kuwa utakuwa kivutio kwa watalii.
Mwanawe Lumumba, Raymond, aliambia BBC kuwa babake angefurahia sana uamuzi wa serikali kujenga mji huo.
"alitaka Congo kuwa kitovu cha maendeleo barani Afrika," alisema Raymond Lumumba.
"kwa hivyo, angetaka uwe mji wa kisasa.''
DR Congo ina utajiri wa madini ingawa watu wengi wanaishi katika umaskini.
Nchi hiyo imekumbwa sana na mizozo kadha wa kadha tangu ijipatie uhuru kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.
Mzozo wa hivi sasa ambao umesababishwa na kundi la M23, ulianza mwaka jana Mashariki mwa nchi na kusababisha takriban watu 800,000 kutoroka makwao.

Wabunge wa Kenya walinganishwa na 'Nguruwe!

Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji waliozingira majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka kujiongeza mishahara.    



Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi pamoja na maji kuwatawanya waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama wa mashirika ya kijamii ambao wamesma katu hawaondoki katika majengo hayo ya bunge hadi wabunge watakapopata ujumbe wao.
Pia inaarifiwa kuwa wanawataka wabunge kutia saini na kuapa kuwa hawatatumia bunge kunyanyasa wananchi maskini kwa kujiongeza mishahara kinyume na sheria.
Mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano hayo kuonyesha ghadhabu waliyonayo wakenya dhidi ya wabunge hao wanaotaka kuongezwa miashara, miezi miwili tu baada ya kufanyiika uchaguzi mkuu wa amani.
Aidha waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye mlango mkuu wa kuingia katika bunge pamoja na damu kama ishara kuwa wabunge ni watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia makubwa.
Maandamano haya yanakuja siku moja baada ya tume ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu wake ni kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu haitawaongeza mishahara wabunge.
Tume hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wabunge hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara lakini hawakufua dafu.
Ni baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge wa Kenya wanataka kulipwa mshahara wa shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la kumi ikipuuza mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi 532,000. Wanasema pesa hizi ni kidogo sana.

Tuesday, May 14, 2013

Mgomo wazuka mgodini Afrika Kusini

Kuna hofu kuwa huenda maandamano kama yaliyoshuhudiwa mwaka jana yakatokea
Kampuni ya uchimbaji madini ya Lonmin, nchini Afrika Kusini inasema kuwa maelfu ya wafanyakazi katika mgodi wake wa wa platinum wamefanya mgomo kinyume cha sheria baada ya afisa wa muungano wao kupigwa risasi katika baa moja mwishioni mwa juma.

Msemaji wa kampuni hiyo Sue Vey amesema kuwa shughuli zote za uzalishaji kwenye kiwanda hicho zimevurugika .                                                                                             
Mgomo huu umezua hofu ya vurugu zaidi kutokea baada ya sekta hiyo kukumbwa na migomo mwaka jana
Mwezi Agosti mwaka jana wafanyakazi thelathini na wanne waliuliwa na polisi katika mgodi wa Marikana na waandishi wa habari wanasema mgomo huo umesababisha hofu ya kutokea kwa ghasia kufuatia hali ya taharuki iliyopo juu ya kukatwa kwa kazi , mashauriano ya riba na uhasama ndani ya muungano wa wafanyakazi.
Lonmin, ambayo hisa zake,ziko katika soko la hisa la London na Johannesburg , ndiyo kampuni ya tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya platinum.
Taarifa za mgomo wa leo zimesababisha hisa za kampuni hiyo kushuka kwa asilimia 5% mjini London.
Msemaji wa kampuni hiyo, Sue Vey alisema kuwa migodi yote kumi na mitatu ya kampuni hiyo imefungwa kwa sasa.
"Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliwasili kazini ingawa hawakuelekea katika shughuli zao kama ilivyo desturi yao
Huku akisema kuwa kampuni hiyo haielewi kwa nini wafanyakazi wameamua kugoma, msemaji wa chama cha wafanyakazi hao, alisema kuwa huenda mgomo huo unatokana na ghadhabu ya wafanyakazi hao, kuhusu mauaji yaliyotokea mwishoni mwa wiki ya kiongozi mmoja wa chama hasimu cha wafanyakazi.
Polisi walithibitisha kuwa kiongozi huyo aliuawa mwishini mwa wiki katika eneo Rustenburg.

Saturday, May 11, 2013

HISTORY YA MWANA HARAKATI BOB MARLEY!



Bob Marley was a hero figure, in the classic mythological sense. His departure from this planet came at a point when his vision of One World, One Love -- inspired by his belief in Rastafari -- was beginning to be heard and felt. The last Bob Marley and the Wailers tour in 1980 attracted the largest audiences at that time for any musical act in Europe.
Bob's story is that of an archetype, which is why it continues to have such a powerful and ever-growing resonance: it embodies political repression, metaphysical and artistic insights, gangland warfare and various periods of mystical wilderness. And his audience continues to widen: to westerners Bob's apocalyptic truths prove inspirational and life-changing; in the Third World his impact goes much further. Not just among Jamaicans, but also the Hopi Indians of New Mexico and the Maoris of New Zealand, in Indonesia and India, and especially in those parts of West Africa from wihch slaves were plucked and taken to the New World, Bob is seen as a redeemer figure returning to lead this.
In the clear Jamaican sunlight you can pick out the component parts of which the myth of Bob Marley is comprised: the sadness, the love, the understanding, the Godgiven talent. Those are facts. And although it is sometimes said that there are no facts in Jamaica, there is one more thing of which we can be certain: Bob Marley never wrote a bad song. He left behind the most remarkable body of recorded work. "The reservoir of music he has left behind is like an encyclopedia," says Judy Mowatt of the I-Threes. "When you need to refer to a certain situation or crisis, there will always be a Bob Marley song that will relate to it. Bob was a musical prophet."
The tiny Third World country of Jamaica has produced an artist who has transcended all categories, classes, and creeds through a combination of innate modesty and profound wisdom. Bob Marley, the Natural Mystic, may yet prove to be the most significant musical artist of the twentieth century.
Bob Marley gave the world brilliant and evocative music; his work stretched across nearly two decades and yet still remains timeless and universal. Bob Marley & the Wailers worked their way into the very fabric of our lives.
"He's taken his place alongside James Brown and Sly Stone as a pervasive influence on R & B", says the American critic Timothy White, author of the acclaimed Bob Marley biography CATCH A FIRE: THE LIFE OF BOB MARLEY. "His music was pure rock, in the sense that it was a public expression of a private truth."
It is important to consider the roots of this legend: the first superstar from the Third World, Bob Marley was one of the most charismatic and challenging performers of our time and his music could have been created from only one source: the street culture of Jamaica.
The days of slavery are a recent folk memory on the island. They have permeated the very essence of Jamaica's culture, from the plantation of the mid-nineteenth century to the popular music of our own times.
Although slavery was abolished in 1834, the Africans and their descendants developed their own culture with half-remembered African traditions mingled with the customs of the British.
This hybrid culture, of course, had parallels with the emerging black society in America. Jamaica, however, remained a rural community which, without the industrialisation of its northern neighbour, was more closely rooted to its African legacy.


Friday, May 10, 2013

Thursday, May 9, 2013

Soma Shairi la Hoja za kijanja kutoka kwa Songa Hapa!






                                                                         [Intro] 

                                                               Yeaah… Duke Tachez.. yeeah
                                                                     [Ubeti wa Kwanza]

                                                                  [Ubeti wa Kwanza]
                                             Yeah, kwa uzima nafungua kinywa nachomoa hii habari
                                                    Naisoma kwa kina vina vinatoboa ka’ bikari
                                                     Nimepima homa kwenye roho ya hii sayari
                                                     Wanasema n’na ngoma eti nakohoa mistari
                                                     Sihitaji support kupost stanza nia
                                                     Verse ni lugha mbili ka’ noti ya Tanzania
                                                     Vibaraka wana njaa, bosi anawaza mia
                                                     Ni mkosi balaa, kitaa tozi anatanga njia
                                                     Mbwiga hasifiki kwa ubingwa wa busara
                                                     Ukiona giza na jogoo haliwiki ujue mida ya kulala
                                                     MC vipi? Mbona huwakilishi shida ya fukara?
                                                    Au umeshapata tija umesahau tiba uchwara?
                                                    Mdomo… hauachi tathmini ya amani ya mswaki
                                                    Mtoa roho angepokea rushwa maskini gani angebaki?
                                                    Stuck kwenye move mi’ ni mkali kwenye flow
                                                    Na-scratch maujuzi m’ ni chaki we ni black wall
                                                    Mzungu anaiga kwenye shida ndugu Mungu,
                                                    Narusha machungu zaidi ya miba ya nungunungu
                                                    Nyoa dungu huu ni msiba mbwiga tubu
                                                    Nimeshika rungu nyumbu anasinywa ka’ sungusungu!
                                                                               [Kiitikio x2]

                                                                           Niite SONGA!
                                                                       Kanuni ya harakati,
                                                     Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati,
                                                                          Niite SONGA!
                                                               Thamani ya muwajibikaji,
                                                   Maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji

                                                                           [Ubeti wa Pili]
                                                                 Wazazi wanasema nimeshakua
                                                      Ina maana… vibaya na vyema nimeshajua
                                                         Jua linazama tazama inanyesha mvua
                                               Nakesha kwa dua kumuombea anayekesha akivua
                                                           Alfajiri inafika na mwezi unazama
                                                      Jogoo la Mbishi lawika na wezi wanahama
                                                      Yamaanisha zienzi tenzi kwa ujenzi salama
                                                 Uweze chutama japo kuna washenzi wanabana
                                                    Wanasema mi’ ni mkali ila why sisikiki?
                                                   Bei ya sukari inafanya ninywe chai na pipi
                                                         Rafiki… mnafiki hanifai kwa dhiki
                                                    N’nachomshukuru Mungu tu uhai silipii
                                                    Cheza pazuri, ukiweza eneza kauli
                                           Wajinga wanatoa macho ka’ wamepoteza nauli
                                               Tenzi shule kwa hizi tungo nikumbuke
                                           Hizi verse nagawa bure kwenye midundo ya Duke

[Kiitikio x2]
[Ubeti wa Tatu]
Baba ananiambia… Maneno hayavunji kuti
Sawa nachana ila mbona flow zangu hazifumi suti
Mi’ mweusi roho yangu haifugi chuki
Dada anasema usiposoma mdogo wangu utarudi bushi
Meza ukweli kwa pressure uteme uongo
Palla anasema Mhaya nd’o kauleta umeme bongo
Kama husajiliwi jitahidi uchenze ndondo
Mwema Mungu sio Said anayesema ubebe gongo
Sifuri ndio inaanza na moja ndio ya pili
Cha ajabu ya pili inaanza na kwanza inasubiri
Hoja ya kishamba haina haja ya kuijadili
Hii ni hoja ya kijanja pata stanza na akili
Hii mic ni shamba na mimi ndio mkulima
Navuna ninachopanda na ulimi ndio unalima
Hapa utaganda huu sio Umwinyi na Ujima
Mzazi mwambie mwana mjini si pa kupima…
[Kiitikio x2]



Mashairi ya mwana harakati Fid q Sihitaji Marafiki!

    





Fid q

Maisha huja na changamoto nyingi mno, hasa katika kipindi cha ujana. Fid Q anasema,”Urafiki sitaki, hauleti maendeleo; masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu; walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru.” 

[Fid Q - Ubeti wa Kwanza]
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
Udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
Udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

Haijalishi ulikuwa na wangapi, bali wangapi uko nao
Washkaji ambao… kosa lako lao wakati hauna mafao
Wanaokufikiria wewe muda ambao, wenzao walionao
Wanafikiria wengine nd’o wanao, now
Kupata washkaji ukiwa na pesa ni rahisi
Kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi
Mie sikufichi sihitaji urafiki na usupastaa
Uki-hit ndo unang’aa, upishwe u-seat kwenye bar,upewe beat na JR
Kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi Fid ni underground
Siku hizi mabinti wanaoni-miss ni walioni-diss, mie sio mdau
Wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mwanza
Ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za Kwanza
UNIT na Prof Ludi walionifunza kukaza
Kwetu mbali sijui lini nitarudi? Lokua Kanza
Sihitaji marafiki, labda baadae wakitokea
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

[Yvonne - Kiitikio x2]
Sihitaji marafiki, no no no
Sihitaji marafiki, marafiki siwahitaji

[Fid Q - Ubeti wa Pili]
Na usupastaa huwa ni feki, utakung’arisha ukiwa na market
Utakupatia senti, utapita juu ya red carpet
Utageuka Young & Restless, utakupa wanawake
Utakupa ma-fake brethrenz.. kisha utaenda zake
Kwahiyo power, it’s not permanent.. huwa ipo kwa muda tu
Respect your own conglomorete, fikiri kikubwa tu
Masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu
Walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru
Wanazusha najis’kia, so I’m my own best friend
Sikia Fid Q anamsifia Fareed ni bandidu, sio “Yes Man”
Naweza nikakata ringi kiasi cha ku-to-pay attention
Lakini sio tajiri wa ku-afford kuua true friendship
Tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga
Na hizi falsafa double-double ajabu sio kinywa cha mjomba
Sihitaji marafiki, labda baadae wakitokea
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea
[Fid Q - Ubeti wa Pili]
Na usupastaa huwa ni feki, utakung’arisha ukiwa na market
Utakupatia senti, utapita juu ya red carpet
Utageuka Young & Restless, utakupa wanawake
Utakupa ma-fake brethrenz.. kisha utaenda zake
Kwahiyo power, it’s not permanent.. huwa ipo kwa muda tu
Respect your own conglomorete, fikiri kikubwa tu
Masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu
Walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru
Wanazusha najis’kia, so I’m my own best friend
Sikia Fid Q anamsifia Fareed ni bandidu, sio “Yes Man”
Naweza nikakata ringi kiasi cha ku-to-pay attention
Lakini sio tajiri wa ku-afford kuua true friendship
Tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga
Na hizi falsafa double-double ajabu sio kinywa cha mjomba
Sihitaji marafiki, labda baadae wakitokea
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

 [Yvonne - Kiitikio x2]


 
[Fid Q - Ubeti wa Tatu]
Rafiki wa kweli yukoje? Ni mkimya au anayechonga?
Yule aliyekupa jina, au pengine anayekuponda?
Anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?
Au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?
Hakuna adui mbaya ka’ rafiki yako mwenyewe ambaye hajui
Ka’ yupo nawe au yupo kinyume na wewe
Bora adui, kama hachachawi utaenda muomba akuelewe
Ka’ buibui, naweka tandu mtaenda kando mzingue?
Kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo
Inabidi tu uwaache waku-watch kwenye kideo
Unakula nao happy leo, kesho wanamtaka mkeo
Urafiki sitaki, hauletagi maendeleo
Nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama Nature
Wachache niliowafanya wakang’aa wanayaweka maisha yangu in danger
Sihitaji marafiki, labda baadae wakitokea
Aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea
[Yvonne - Kiitikio x2]