Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa mtazamo mkali wa ujumbe wa kulinda
amani wa Umoja wa mataifa ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kagame ameiambia BBC kwamba kikosi cha Umoja wa Mataifa cha askari
elfu 20 kilichopelekwa miaka 14 iliyopita, hakijafanya lolote kutatua
chanzo cha matatizo ya Congo na wakati mwingine kimeufanya mzozo huo
kuwa mmbaya zaidi.
Amesema visa vya mapigano , ghasia, na watu kupoteza makaazi yao kulitishia usalama wa eneo zima.
Serikali ya rais Kagame imekana mara kwa mara
tuhuma za Umoja wa mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba
Rwanda inawasaidia wanamgambo mashariki mwa Congo.
Rais Kagame amesema kuwa kutumia nguvu kungesaidia ikiwa tu inekuwa inalenga kusaidia msimamo fulani wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment